Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

KIMENUKA BUKOBA SOMA HAPA UONE LIVE!!

$
0
0

KAGASHEKI ALIPUKA

 Baada ya kujiuzulu, aweka kambi jimboni
 Asema bora jiwe lichaguliwe kuliko Amani
Vita ya kisiasa inayohusisha mahasimu mawili ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Manispaa ya Bukoba, imeibuka upya, kufuatia ‘taarifa tata’ ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Meya wake, Dk. Anatory Amani.

Mbunge wa Bukoba Mjini (CCM), Balozi Khamis Kagasheki, baada ya kujiuzulu kutoka Waziri wa Maliasili na Utalii, amerejea jimboni humo, na kuendeleza `vita’  inayolenga kumdhibiti Dk. Amani.
Balozi Kagasheki, aliitisha mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa-Mayunga, ambapo aliwapiga vijembe Dk. Amani na viongozi wa CCM na serikali mkoani Kagara.
Pamoja na Dk. Amani, Balozi Kagasheki aliwakosoa   Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe na Katibu wa CCM mkoani humo, Avalin Mushi.
Mashambulizi ya Balozi Kagasheki dhidi ya viongozi hao, yalikuwa sehemu ya tahadhari aliyoitoa kwa ‘wanaojipitisha’ jimboni humo, wakati mwakilishi halisi wa wananchi (yeye) yupo.
Akawaonya waache vitendo hivyo na kwamba yeye (Kagasheki), ndiye mwenye dhamana ya kuwasemea wananchi wa jimbo hilo.
Balozi Kagasheki, alisema kujiuzulu kwake muda mfupi kabla ya Rais Jakaya Kikwete kumfukuza kazi Desemba mwaka jana, hakumnyimi usingizi, kwa vile hakuiomba nafasi hiyo kama ilivyo kwa ubunge wa Bukoba Mjini.
Akionekana kuelekeza nguvu zake jimboni Bukoba Mjini, Balozi Kagasheki, alisema haoni nafasi iliyopo kwa mshindani wake wa kisiasa, Dk Amani, kumshinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
“Yule bwana nilimleta mwenyewe. Nilimchonga mimi na niko tayari kushindana na mtu mwingine lakini si Dk Amani… hata nisipogombea 2015, nafasi yangu ikawekwa jiwe, nitahakikisha jiwe linashinda,” alisema.
TAARIFA YA CAG
Balozi Kagasheki, alisema aliwahi kuujulisha umma kuhusu namna Dk. Amani anavyohusika katika sakata la ubadhirifu ulioibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Ludovick Utouh.
Alisema pamoja na tahadhari hiyo, alipendekeza Dk. Amani kujiuzulu nafasi ya umeya kwa vile miradi mingi yenye utata ilionyesha ushiriki wake kama ilivyothibitishwa na CAG.
AWASHUKIA MASSAWE, MUSHI
Balozi Kagasheki, aliwashutumu hadharani Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Massawe na Katibu wa CCM mkoani humo,  Mushi, kwa kuchafua hali ya kisiasa jimboni mwake.
Alisema maendeleo ya watu wa Bukoba yataletwa na wakazi wa Bukoba na si vinginevyo.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Kagasheki ilikosolewa na baadhi ya watu, wakiihusisha na ‘mbegu ya ukabila’ dhidi ya watendaji hao wenye asili ya mkoani Kilimanjaro.
Balozi Kagasheki, alisema kama viongozi hao (Massawe na Mushi) hawawezi kuachana na ‘kumchafulia’ jimboni kwake, waondoke mkoani Kagera kumwacha aendeleze siasa na kushirikiana na wananchi kujiletea maendeleo yao.
KAULI MBIU YA MAENDELEO YABADILISHWA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wapambe wa Balozi Kagasheki, walibadilisha kaulimbiu ya mkoa inayosema, ‘amani na maendeleo’, badala yake wakaitamka kuwa ‘haki na maendeleo’.
Kauli mbiu ya awali, ilihusishwa na neno la kwanza-amani, kufanana na jina la Meya mwenye taarifa za utata kuhusu kujiuzulu kwake, Dk. Amani.
Japokuwa  kaulimbiu hiyo ilihamasishwa katika wilaya zote za mkoa huo na Kanali mstaafu Massawe, lengo likiwa ni kuhamasisha amani na maendeleo, jana zilipingwa na wafuasi wa Balozi Kagasheki.
Hata hivyo, mabadiliko ya kauli mbiu hiyo hayakupokewa vizuri na baadhi ya wakazi wa mjini hapa, wakielezea kwa nyakati tofauti kuwa ni kielelezo cha ubabe na kuwadharau viongozi wengine.
Hivi karibuni, kulikuwapo na taarifa za kujiuzulu kwa Meya huyo, ambaye hata hivyo alijitokeza hadharani baada ya siku kadhaa, akikanusha kuhusu tukio hilo.
NIPASHE

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>