Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

SUPER STAR SHAA WA BONGO FLEVA AWASHUKIA WASANII WANAJIKWEZA LIVE!!

$
0
0

 

  • Kupitia mahojiano na Starehe mwanzoni mwa wiki, Shaa ambaye jina lake halisi ni Sarah Kaisi anaeleza kuwa wasanii wengi nchini wamekuwa wakiacha kufanya muziki utakaowanufaisha na kukimbilia kurekodi na wasanii wakubwa, huku wakipoteza fedha nyingi ambazo wangewekeza katika muziki wa hapa nyumbani na kufaidika zaidi.

Wakati baadhi ya wasanii wa kiume wakichachamaa kurekodi nyimbo zao wakishirikiana na wanamuziki wakubwa wa kimataifa(kolabo), msanii wa kike katika muziki nchini Shaa, amesema kuwa hawezi kufanya jambo kama hilo na staa yeyote wa nje bila kuwa na hakika kwa manufaa upande wake.
Kupitia mahojiano na Starehe mwanzoni mwa wiki, Shaa ambaye jina lake halisi ni Sarah Kaisi anaeleza kuwa wasanii wengi nchini wamekuwa wakiacha kufanya muziki utakaowanufaisha na kukimbilia kurekodi na wasanii wakubwa, huku wakipoteza fedha nyingi ambazo wangewekeza katika muziki wa hapa nyumbani na kufaidika zaidi. Endelea…
Starehe: Wasanii wengi sasa wanafanya kolabo za kimataifa, vipi upande wako una mpango gani mwaka huu?
Shaa: Siwezi kufanya kolabo na staa yeyote wa kimataifa, mimi nipo kibiashara zaidi na ni ngumu kwangu kwa sababu nahitaji kufanya muziki nipate fedha. Hizi kolabo za kimataifa unajikuta ukimlipa pesa mhusika huku wewe ukiingia gharama ya kusafiri huko na kurekodi. Kama unavyojua, inachukua muda na gharama kubwa, nahitaji kufanya kitu ambacho nitafaidika nacho na siyo kunipotezea fedha.
Starehe: Wasanii wa kiume wamejitahidi kufanya kolabo na mastaa wakubwa wa nje unadhani wanafaidika katika hilo?
Shaa: Inategemea, lakini asilimia kubwa kolabo hizo ni za kulazimisha na kupoteza pesa, siyo za kuuza au kumwingizia kipato mhusika. Unatakiwa ufanye kolabo, kisha upate shoo kubwa za kurudisha gharama uliyotumia. Lakini nionavyo mimi nyingi ni za kutafuta ujiko tu, siwezi kufanya kolabo na D Banj kisha isiniingizie chochote.
Starehe: Wanamuziki wa kike wana nafasi katika soko la sanaa hapa nchini?
Shaa: Wanamuziki wa kike tuna nafasi kubwa zaidi. Hii ni tofauti na wenzetu wa kiume, lakini tunashindwa kuitumia hiyo nafasi, Tunapaswa kujiweka kibiashara zaidi, lakini wengi wanauza sura tu na kulazimisha muziki. Muziki unataka kujipanga na kujinoa kila wakati, lakini walio wengi wanaimba kwa mazoea na hawataki kubadilika.
Starehe: Unadhani nini kinasababisha wasanii wa kike kuibuka na kupotea sokoni baada ya muda mfupi?
Shaa: Ubunifu ni suala nyeti lenye matokeo chanya siku zote, lakini wengi hawana muda huo na wanashindwa kuchukulia muziki kama kazi. Mtu akiwa staa anajiendeleza katika mambo mengine na siyo kuwa bize na muziki uliompa nafasi ya juu. Sasa mtu anaimba kila siku hana mabadiliko, muziki ni kama chakula, inafikia hatua kinamkifu mtu, au kama Big G utamu ukiisha unaitema. Tofauti na wenzetu Ulaya, ukiangalia kila albamu ya mwanamuziki Beyonce au Rihanna ina ladha tofauti na sauti yenye upekee.
Starehe: Hii ndiyo sababu iliyokufanya ukabadili staili ya uimbaji wako?
Shaa: Ndiyo, katika uimbaji wangu sikuegemea sehemu moja, siyo kwamba siwezi kufanya, bali mimi ni msanii, lazima nibadilike. Ndiyo maana nimeweza kuimba Kwaito, Mduara na ninaweza kuja na muziki wa Injili pia. Hii haitamaanisha kwamba nimeingia kwenye muziki huo moja kwa moja, mimi ni msanii mwenye uwezo wa kubadilika kutokana na wakati.
Starehe: Kwa kipindi kirefu umekuwa ukiimba muziki wa aina tofauti, umepokewa vipi na mashabiki ulipoimba wimbo wa Sugua Gaga, ulioimba mtindo wa mduara?
Shaa: Wimbo huu niliimba kwa nia ya kuwafurahisha zaidi watu wa uswahilini, lakini kwa bahati nzuri umepokewa vyema hata uzunguni, yaani wameuelewa sana. Pia ni wimbo uliotazamwa zaidi katika mtandao wa You Tube kuliko nyimbo zangu zote nilizowahi kuimba. Umeniletea umaarufu mkubwa na kuniongezea mashabiki katika ukurasa wangu wa Facebook. Zaidi, umenipatia shoo nyingi tangu niutoe kwa mara ya kwanza Novemba 1 mwaka jana. Sikutegemea lakini imeweza pia kushika namba moja kwenye vyombo vya habari Afrika Mashariki.
Starehe: Mashabiki wategemee kupata nyimbo ya Injili kutoka kwako kwa mwaka huu?
Shaa: Itakuwa ni papo kwa papo, ninahitaji kuwashangaza tu nitakapoachia wimbo wangu mwingine mapema mwezi Machi maana kwa sasa ni mapema mno na Sugua Gaga bado inafanya vizuri sokoni.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>