Wiki iliyoisha tulipata muda wa kukaa na Producer Luciano Tsere aka LuccidaDon au unaweza kumuita lucci na kufanya naye maojiano kadhaa kuhusiana na muziki anaofanya , kazi yake ya music production na zaidi ya yote mahusiano yake yeye na jokate na feza kessy. kwa kifupi lucci amezaliwa tarehe 30 September 1985 Lusaka Zambia, akiwa ni mzaliwa wa nne, wa mwisho kuzaliwa na akiwa mtoo wa kiume pekee kwenye familia.
kuhusiana namahusiano yake na feza kessy lucci aliyasema haya “Nilikuwa na uhusiano na Feza, i event engaged her mwaka 2012, na kuna kazi nyingi ambazo nimeshawahi kumfanyia kimziki, bahati mbaya tulikuja kuachana, tulikuwa pamoja for 2 years, actually moja ya sababu iliyofanya tuachane ni kwamba unajua kuna kuvumiliana na kupeana chances, alivoingia big brother mimi sikuwa na tatizo ila alivoanza niongelea vibaya mimi na familia yangu in public hiyo sikupenda kwakweli, unajua nnafahamiana na watu wengi, en kuna watu walikuwa wanafahamu kuhusu uhusiano wetu sasa kuanza kuongeleana vibaya sikupenda kwakweli”