Mhe. Abdulkarim Shah, Mbunge wa Mafia, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamishna wa Tume ya Utumishi ya Bunge, anasikitika kutangaza kifo cha mama yake mzazi, Bi. Fatma Abdulkarim Mussa (pichani) kilichotokea Chennai, India tarehe 28 Januari, Mwili wa marehemu utawasili nchini tarehe 30 Januari, 2014 kwa ndege ya Shirika la Emirates, saa tisa alasiri na kuzikwa siku ya Ijumaa saa saba mchana katika makaburi ya Kisutu.
Msiba upo Magomeni, Mtaa wa Matombo, Mwembechai karibu na kwa Sheikh Yahya Hussein.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:
1. Mhe. Abdulkarim Shah - +918 015 026 119 (India)
2. Ndg Khalid Shah - 0715 567865
3. Ndg. Athumani Kwikima - 0759 683 421 - 0787 965 965/0759 305 739
Source:- Michuzi Blog