Mwanamitindo anayefanya vizuri sana nchini, Danny David atazindua kampuni yake mpya ya Gracing Africa inayojihusisha na ukuzaji na uendelezaji wa vipaji nchini hasa vya mitindo na fashion ijumaa hii katika hoteli ya Serena ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa meya wa jiji la Dar es Salaam mheshimiwa Jerry Slaa.
Uzinduzi huo wa aina yake utakuwa wa mwaliko pekee ni watu wachache watakaochaguliwa kuhudhuria sherehe hiyo.
Danny ambaye hivi karibuni amerejea nchini toka nchini Afrika ya kusini alipoenda kwa ajili ya shuguli za kizazi amesema lengo la kampuni hiyo ni kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wengi nchini katika lengo la kuboresha maisha yao.