Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza mhifadhi wa Sokwe wa kimataifa Dkt.Jane Goodall wakati mhifadhi huyo alipomtembelea Rais Ikulu na kumwelezea kazi zake mbalimbali za uhifadhi nchini.Dkt.Goodall anajihusisha na uhifadhi wa Sokwe katika hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma na kazi yake imeipatia Tanzania umaarufu mkubwa Duniani.Dkt. Goodall ni mwanzilishi wa taasisi ya Jane Goodall Institute inayojihusisha na uhifadhi wa Sokwe. Picha na Freddy Maro
↧