MSHAMBULIAJI Shaaban Kondo wa Yanga amejiunga na kikosi hicho baada ya kuachiwa huru na jeshi la polisi juzi.
Kondo alikamatwa na polisi wakati akiingia ndani akitokea jukwaani kuwafuata wachezaji wenzake waliokuwa wanacheza kutokana na askari kutomtambua na yeye kutokuwa na kitambulisho wala sare za timu.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuto alisema mchezaji huyo aliachiwa huru juzi jioni baada ya uongozi kuzungumza na Jeshi la Polisi Kanda ya Temeke.
"Yupo huru tangu jana “juzi” na ameshaungana na wenzake baada ya uongozi kuzungumza na Jeshi la Polisi kanda ya Temeke," amesema Kizuguto.
Kondo aliyesajiliwa na Yanga msimu huu alikamatwa baada ya mchezo wa raundi ya 16 dhidi ya Mbeya City na Yanga kushinda kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.