MWANASOKA bora wa Dunia Cristiano Ronaldo alipewa kadi nyekundu ya utata wakati Real Madrid pungufu ya mchezaji mmoa ikilazimishwa sare ya 1-1 na Athletic Bilbao jana Uwanja wa San Mames katika La Liga.
Mshambuliaji huyo alitolewa nje baada ya kumuwakia Carlos Gurpegi na baadaye kugombana na Ander Iturraspe dakika ya 75.
Dakika moja kabla, Athletic walipata bao la kusawazisha lililofungwa na Gomez aliyetokea benchi kufuatia Jesse kuifungia Real bao la kuongoza dakika ya 65.
Matokeo hayo yanaifanya Real itimize pointi 54 na kubaki nafasi ya tatu katika msimamo wa La Liga, baada ya kucheza mechi 22, nyuma ya Barcelona yenye pointi 54 pia.
Ushindi wa maba 4-0 wa Atletico Madrid jana dhidi ya Real Sociedad unawapandisha kileleni baada ya kutimiza pointi 57 katika mechi 22 pia. Shukrani kwao David Villa, Diego Costa, Miranda na Diego waliofunga mabao hayo Uwanja wa Vicente Calderon