Wengi waliosikia kuna wimbo wa Shakira na Rihanna unakuja walipata hamu ya kujua muunganiko wa hivi vichwa utakuwaje?
Kolabo hii ilipotoka, muda mfupi baadae ilianza kupokea maoni mbalimbali yakiwemo ya kusifia mavazi, muonekano, huku mengine yakihusisha video hii na kampeni ya kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.
Tayari mwanasiasa maarufu nchini Colombia anakotokea Shakira, Marco Fidel Ramirez amekua miongoni mwa walioikosoa kwa kutaka mamlaka ya urushaji wa matangazo ya Television nchini humo iifungie hii video kwa sababu imekosa maadili, inaonekana kuunga mkono kampeni ya mapenzi ya jinsia moja.
Anasema pia hii video inaweza kushawishi watu wenye udhaifu kuingia kwenye mapenzi ya jinsia moja, ni video ya hatari ambayo pia inachochea matumizi ya tumbaku na vitu vingine vibaya.