- Ni kauli ya waziri , ikilenga kurudisha hadhi ya wizara na kuokoa mifugo.
Dar es Salaam.Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk Titus Kamani amesema, Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wataalamu wa mifugo wanaojihusisha na utengenezaji wa chanjo bandia.
Akizungumza na wataalamu wa mifugo katika Kiwanda cha Taifa cha Uzalishaji Chanjo kilichopo Kibaha mkoani Pwani, Dk Kamani alisema endapo itabainika kuna wafanyakazi wasiofuata maadili na kujihusisha na vitendo vya utengenezaji wa chanzo bandaia atahakikisha anaishia gerezani.
Kauli hiyo ya Dk Kamani imekuja baada ya kiwanda hicho kufungiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kutokana na tuhuma za kutengeneza chanjo bandia na huku nyingine zikiwa chini ya kiwango hali inayosababisha wafugaji kupata hasara kwa kupoteza mifugo yao.
Alisema, wakati umefika sasa kwa watumishi wa wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kila mmoja kwa nafasi yake kutafuta njia zitakazosaidia kuongeza uzalishaji mali.
“Hatuwezi kuwavumilia watumishi ambao wanakiuka miiko ya kazi yao na kutengeneza chanjo bandia hali inayosababisha wafugaji kupata hasara, endapo wapo watakaobainika nitahakikisha wanakwenda gerezani wala hatutakuwa na muda wa kuwasimamisha kwa ajili ya uchunguzi,”alisema Dk Kamani.
Dk Kamani aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanazingatia upungufu wote ulioainishwa na TFDA na maelekezo waliyopewa ili kuhakikisha chanjo inayotengenezwa inakidhi viwango vya ubora.
Kaimu Mtendaji wa kiwanda hicho, Dk Furaha Mramba alisema kiwanda hicho kinahitaji fedha za Kitanzania Sh250 milioni ili kuanza upya uzalishaji wa chanjo baada ya kufuata maelekezo yote ya TFDA.
“Tumejaribu kuchukua hatua kadhaa ikiwamo kuwahamisha wafanyakazi waliokuwapo awali na kuwaleta wapya, tunaendelea kuwasiliana na TFDA kinachotukwamisha kwa sasa ni fedha,”alisema