Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

HABARI KAMILI ON SUPER STAR DR. CHEN NA FREEEMASONS SOMA HAPA LIVE!!

$
0
0

MINONG’ ONO na uvumi unaotambaa kwa kasi kuwa anajihusisha na taasisi ya wajenzi huru (Freemasons ), unazidi kumtesa msanii wa filamu za Kibongo , Mahsein Awadhi Said ‘Dk . Cheni ’ kwa madai ya kwamba anajisikia vibaya anaponyoshewa vidole na baadhi ya wadau wa tasnia hiyo .

Dk . Cheni . Mwishoni mwa wiki iliyopita , mwandishi wetu alisikia fununu kutoka kwa wadau wengi wa filamu wakiwemo wasanii wenzake wakidai kuwa Dk . Cheni ni mwanachama halali wa taasisi hiyo ndiyo maana mambo yake ni mazuri kifedha ukilinganisha na wasanii wengine wanaoaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kuigiza kuliko yeye . “ Kila dalili inaonesha kabisa Dk . Cheni ni Freemason , angalia mavazi yake mengi ni meusi , machata na alama kibao zinazohusishwa na taasisi hiyo, angali fedha aliyonayo, angalia hata gari lake lilivyojaa alama za ajabu ajabu, huyu jamaa ni Freemason kabisa , ” alisema mdau mmoja wa filamu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alipozungumza na mwandishi wetu .

 Kauli kama hizo zimekuwa zikitolewa kwa nyakati tofauti na baadhi ya wasanii wenzake . Dk . Cheni alipotafutwa kwa njia ya simu Jumapili ya wiki iliyopita na kuulizwa madai hayo alikuwa na haya ya kusema : “ Dah! na wewe umeyapata kaka ? Hakika naumia sana na madai hayo , yamevuma sana kwa wadau , tena baadhi yao ni watu ninaowaheshimu sana, jamani mimi siyo Freemason , naigiza , kazi zangu za u - MC zinaniingizia kipato, najiwekea akiba . “ Si mtu wa starehe , nawekeza katika biashara ndogondogo, madai haya ya Freemason yananitesa sana ila namwachia Mungu , ” alisema Dk . Cheni .
credit:bongoclantz

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>