Jamani kuna kitu kinaitwa wivu ma ukali vitu hivi huwa haviachani sana kwenye mapenzi, sasa mimi jamani mchumba ninaye tarajia kufunga nae ndoa ni mkali sana. Yani yeye kitu kidogo tu hunikasirikia hata hataki kusikia chochote kutoka kwangu. Hajawahi kunipiga hata siku moja ila kwakweli ukali wake unanitisha na nimeshakaa nae chini kumwambie ajirekebishe lakini imeshindikana, mi naona kama mwishowe nitachoka natabia zake. Naombeni Ushauri Mwenzenu..!!
↧