Waombolezaji wakisukuma jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), marehemu Balozi Fulgence Kazaura ulipowasili leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jioni hii , kutoka India. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick akiwafariji ndugu wa marehemu
Ndugu jamaa na wafanyakazi na aliye kushoto ni Dereva wa gari la kubeba mwili huo wakifunua jeneza kwa utambuzi wa mwili wa marehemu Kazaura mara ulipo wasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jioni hii , kutoka India.
Wakiutoa nje tayari kwa kuondoka uwanjani hapo kupelekwa kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Kairuki, Mikocheni
Mwili ukipakiwa kwenye gari tayari kupelekwa kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Kairuki, Mikocheni,kulia ni dereva wa gari litakalo beba mwili