KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa mbunge au diwani anayetaka kuondoka CHADEMA milango iko wazi, kwa sababu hawawezi kumvumilia kiongozi msaliti wa chama.
Dk. Slaa alitoa msimamo huo jana wakati akimnadi mgombea ubunge wa CHADEMA jimboni Kalenga, Grace Tendega, katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa mnadani, Kijiji cha Kidamali, Kata ya Nzihi huku akisisitiza kuwa hata wakibaki watatu tu ndani ya chama, Chadema haitakufa na kwamba wameridhia kujiuzulu kwa madiwani wao wawili mkoani Shinyanga.
Alisema kujiuzulu kwao ni mpango maalumu uliotengenezwa na wapinzani wao kisiasa kwa lengo la kuwadhoofisha na kuwavuruga -