Hata siku moja hakuna atakayenishawishi kwamba kura muhimu kupitisha Katiba iwe ya siri wakati kura ya kupitisha Bajeti inakuwa ya wazi. Kura ya kupitisha Bajeti linaitwa jina moja moja. Kwenye Katiba iwe hivyo ili tuwajue waliposimama wajumbe wetu na tuwahoji kwa kura zao. Labda walioteuliwa na Rais wapige kura za siri. Mimi ningependa watu wa Bumbuli waijue kura yangu na nikaielezee kwao na niwajibike nayo.
↧