"Nimeamua kutoka nje (kuepusha shari) baada ya Mbunge mwenzangu wa chama cha CUF kunitukana (kaniita mshenzi) kwa jazba baada ya kumsihi asizomee wakati mbunge mwingine anachangia hoja yake bungeni. Hata hivyo nilichojifunza hapa ni kwamba, kama hatutakuwa na dhana ya kuvumiliana miongoni mwetu na kukubali kusikiliza hata lile usilopenda kusikia, basi kwa hakika mkutano huu unaweza usiishie kwenye heri"
↧