Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

UNYAMA WA KUTISHA WA CHADEMAZ KWA WATANZANIA WASIO NA HATIA HUU HAPA

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Ifakara wakati wa Mkutano wa Kufungua Kampeni uliofanyika Jana Tar.27/02/2014.Hapa akiwa na Wahanga wa siasa chafu zinazodaiwa Kufanywa na Chadema kupitia Vijana wake wa Redbrigade.Mwenye T-shirt ya Njano ni Mzee Alphonce John ambaye alitopolewa Macho kwa dispisi wakati wa Uchaguzi wa Udiwani huko Kahama Mwezi uliopita.
Mwigine mwenye Shati la Kijana ni Kijana Musa Tesha ambaye alimwagiwa Tindikali na Vijana wanaodaiwa Kuwa wa Chadema huko Igunga wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo.
Mh:Mwigulu Nchemba jana amesisitiza Wananchi wa Kalenga kuwa makini na siasa Chafu za Chadema zinazofanywa sehemu mbalimbali hasa kwenye nyakati kama hizi za Uchaguzi.Amesisitiza kuwa kwenye Chaguzi zozote Vyama vya siasa vinashindanisha Sera na hoja kuhusu Maendeleo ya Wananchi wa eleo hilo,Mkataba wa CCM na Wananchi ni Maendeleo katika Taifa hili,Umoja na Mshikamano ndio ngao ya MwanaCCM yeyote.
Mwigulu Nchemba amesema dhambi ya Mauaji na Unyama unaoendelea kwenye mikutano ya siasa na maeneo mbalimbali haitamwacha Dr.slaa Salama kutokana na yeye kuwa kiongozi anayebariki Siasa chafu hizo.
Chanzo:Kalenga

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles