Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

WILLIAM KAIJAGE AICHAMBUA DHANA YA KUZIMWA KWA SIMU FEKI LEO USIKU SOMA HAPA LIVE!!

$
0
0
William Kaijage's photo.
SIMU “FAKE”…
•Kutokana na kufanya kazi kwenye telecom industry kwa muda mrefu, watu wengi wamekuwa wakiniuliza maswali kuhusu hili zoezi la uzimaji wa simu “fake” saa 6 ya usiku wa Alhamis (16-Jun-2016) kuamkia Ijumaa (17-Jun-2016). Nitazungumzia maswali ma-3 ambayo yanajitokeza zaidi.


1. HIVI NINI FAIDI YA KUZIMA SIMU? TAIFA LINAPATA FAIDA GANI LIKIFUNGIA SIMU? AU KUNA HASARA GANI SIMU ZISIPOZIMWA?
Lengo kubwa la mchakato huu ni kusaidia hapo baadaye kudhibiti uhalifu. Hii inaweza kuzungumziwa kwa namna 2;

•Wizi wa Simu: Kwa utaratibu utakaokuja, simu ikiibiwa na ikaripotiwa, itakuwa inafungiwa isitumike kwenye mtandao wowote hapa Bongo. Kwa utaratibu uliopo hivi sasa, hilo lilikuwa halitekelezeki. Kwa hapa Afrika, South Africa utaratibu huo unafanya kazi.

•Crime Tracking: Mhalifu akijulikana anatumia namba fulani, itakuwa ni rahisi kuzijua namba zingine zote ambazo huzitumia kwenye simu yake. Pia akibadili SIM card yake na kuweka kwenye simu nyingine, mawasiliano yote pia ya simu hiyo nyingine itakuwa rahisi kuyafuatilia kwa kushirikiana na kitengo cha Cyber Crime cha Police.

Simu zikiwa na genuine EMEI number inakuwa rahisi ku-control uhalifu. IMEI number (International Mobile Station Equipment Identity) ni namba unique ambayo hu-identity vendor (eg Samsung, Tecno) na device kwa mujibu wa Internation Standards.

2. HIVI ZITAKAZOFUNGIWA NI SIMU FAKE AU SIMU ZENYE INVALID IMEI NUMBER

•Kusema kweli zoezi hili halihusiani kabisa na simu feki. Sio rahisi kupambana na simu feki. Simu fake ni ile ambayo brand does not match the hardware (aka clone). Zipo clone nyingi zenye valid IMEI.

•INVALID IMEI zina-include Blanks, duplicates, blocked, non-issued au wrong format.

•Kifaa kinachotumika na TCRA kutambua hilo kinaitwa Integrated Identiry Register (IIR) ambayo huunganisha Identity Registeres (IR’s) za makampuni ya simu (Mobile Operators)

3. NASIKIA SUALA LA SIMU KUFUNGIWA SIMU LINATOKANA NA MAKAMPUNI MENGI YA SIMU KUTOLIPA KODI KWA HIYO WANATAKA KUYABANA

•Sio kweli. Zoezi hili halihusiani na jitihada zozote za kupambana na kutolipa kodi. Zoezi hili linahusiana na uhalifu zaidi. Maswala ya kodi ni jambo tofauti.
 

•TCRA mwezi March-2014 walizindua Telecommunications Traffic Monitorring Systems (TTMS) pale Makao Makuu ya TTCRA jengo la Mawasiliano. Mtambo ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete.
 

•Ila mtambo huu una-track simu za kimataifa tu (international calls).
 

•Sababu kubwa ya ukwepaji wa kodi ni kwa vile TCRA hadi hivi sasa haija-implement system yak u-track local traffic. Hii haina uhusiano na Identiry Register (IR) au usahihi wa IMEI number.
 

•Kuchelewa kwa implementation ya hii kitu kulitajwa kama moja ya sababu iliyosababisha rais JPM kutengua u-DG wa TCRA (Dr Ally Yahya Simba) mwezi April mwaka huu.

MENGINEYO
 

•Takwimu zinaonyesha ni 2% tu ya simu ndio zitafungiwa (kwa mujibu diagram niliyoiweka)
 

•Makampuni ya simu kama TIGO yameanza utaratibu wa kujiandaa na any possible revenue loss kwa kutoa simu bure in exchange of simu “fake”
 

•Njia pekee ya kujua kama simu ni “fake” ilikuwa na kupitia SMS na kupitia tovuti yao

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>