Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

LE MUTUZ LIVE STRAIGHT TALK WABUNGE WOTE WASIOTAKA KURA ZA WAZI HUKO DODOMA BUNGE LA KATIBA NI COWARDS!!

$
0
0

Default Wabunge Wote Wasiotaka Kura za Wazi are Cowards ni wakati Muafaka Wakajitoa huko Dodoma Haraka Sana!

- Nimeshitushwa sana na habari za mzozo wa Kupiga kura huko Dodoma kwenye bunge la Katiba, siamini kwamba leo 2014 Tanzania tuna viongozi watuwazima na akili timamu wanalia lia kama watoto wadogo eti wanaogopa kupiga kura za wazi are you kidding me or what? Katika kuishi kwangu nje miaka mingi sana sijawahi kusikia Viongozi wanaume wakililia kupiga kura za siri on anything, sasa sisi Tanzania tumemkosea nini Mungu mpaka kuweza kuwa na Viongozi wa Taifa waoga waoga mpaka kuogopa kupiga kura ya wazi?

- Mimi nilidhani Wanasiasa wote Duniani huwa wanalilia kazi zao kuonekana wazi kwa wananchi na hizi kura ndio haswa ilikuwa nafasi za wanasiasa wetu kuonyesha misimamo yao wazi kwenye kura na kuweza kusimama kuitetea kwa nini wamepiga kura kama walizopiga, badala yake naona wanaume watuwazima wakilia lia kila siku kuomba wapige kura za siri kusudi wasijulikane na wananchi wanaowaongoza wamepigaje kura zao, Really?

- Naomba wale Viongozi wote huko bungeni Dodoma wanaolilia kama watoto habari za kupiga kura za siri waondoke huko mara moja, cause hawafai, ni kiongozi gani Duniani leo anayeogopa kupiga kura ya wazi na kusimama mbele ya Taifa kutoa sababu za kwa nini amepiga kura yake kama alivyopiga? Ukweli ni kwamba hawafai kuwa Viongozi na hata kuwa wawakilishi wa wengine, wananchi wa Tanzania hatujawatuma viongozi waoga na cowards huko Dodoma ni simply kwamba hawawezi na hawatufai, waondoke mara moja na wawaachie wananchi wengine nafazi zao, wananchi wasio ogopa kuhesabiwa na umma!!, Wananchi tunataka katiba mpya na inatakiwa kuandikwa na wananchi walio tayari kufa kwa kusimamia misimamo yao, sio waoga waoga kama fisi fukuza wote huko Dodoma waoga waoga!!

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA

Le Mutuz Big Show


Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>