Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

SAFARI YA MECHI YA MARUDIANO MISRI YANGA YAWEKA CHINI MSIMAMO WAKE LIVE!!

$
0
0

  • Yanga na Ahly zitarudiana mjini Cairo Jumapili ijayo, katika mechi ya kwanza Yanga ilishinda.

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Van Der Pluijm amesema timu yake haitakwenda Misri ikiwa na dhana ya kwenda kujilinda ila itashambulia muda wote kwa lengo la kusaka mabao.
Yanga na Al Ahly zitashuka uwanjani kukabiliana katika pambano la marudiano litakalopigwa Jumapili hii jijini Cairo, Misri.

Katika pambano la kwanza lililopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga ilichomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly.
Pluijm alisema staili ya kushambulia muda wote ambayo kikosi chake kiliitumia katika pambano la kwanza ndiyo atakayoitumia ugenini Misri.
“Jambo la kwanza tutamiliki mpira halafu tutashambulia muda wote kama tulivyofanya nyumbani, kama tukienda kucheza soka la kujilinda kwa sababu ya bao moja hapo tutakuwa tunajidanganya kwani katika soka njia sahihi ya kuzuia mashambulizi ni wewe kumshambulia adui,”alisema Pluijm.
Alisema,”Tumetengeneza nafasi nyingi katika mchezo wa kwanza, lakini tuimetumia moja tu, nafikiri tutaongeza umakini zaidi katika mchezo wa marudiano kwa kuhakikisha kila nafasi tutaitumia.”
“Nikiri kwamba mbinu tuliyoingia nayo katika mchezo wa kwanza ilifanikiwa, utaona Emmanuel Okwi alikuwa anacheza kama mshambuliaji pekee, Mrisho Ngassa nyuma yake huku tukiwa na mawinga Simon Msuva na Hamis Kiiza na ndio maana tulitengeneza nafasi nyingi,”alisema Pluijm.
Naye kocha msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa alisema watawaandaa wachezaji wao kisaikojia na kimwili kwa ajili ya kukabiliana na mizengwe ambayo inaitarajiwa itajitokeza katika pambano la marudiano dhidi ya Al Ahly.
Mkwasa alisema kuwa timu yake inafahamu itakutana na changamoto ya mizengwe katika pambano la marudiano, hivyo wamejiandaa kukabiliana nayo.
“Tunafahamu kwamba mechi ya marudiano itakuwa na mizengwe mingi, lakini benchi la ufundi litawaandaa wachezaji kisaikolojia na kimwili kwa ajili ya kukabiliana na hali hiyo,”alisema Mkwasa.
Wakati huo huo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amewataka wachezaji wa Yanga kutobabaishwa na mizengwe katika pambano la marudiano na badala yake waelekeze akili zao kusaka ushindi.
“Hivi karibuni nilikuwa Misri na nilishuhudia mechi kati ya Al Ahly na Sfaxien ya Tunisia, wale jamaa wamezoea mambo ya ajabu ajabu kama kulipua baruti au kuwasha miale ya moto na kupuliza filimbi kama ya mwamuzi wakati unaenda kufunga.
“Lakini mimi nasema hayo mambo yasiwababaishe wachezaji wa Yanga kwa sababu uwanjani kuna mtu mmoja tu mwenye mamlaka naye ni mwamuzi atawalinda, wao waelekeze akili zao kusaka ushindi tu na wale wanafungika kabisa hata kwao,”alisema Malinzi.
Kwa upande wake nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Canavaro’ aliwatahadharisha wachezaji wenzake kwa kuwataka wasibweteke na ushindi walioupata katika mechi ya kwanza baina yao na Al Ahly badala yake wajiandaae kikamilifu kwa ajili ya mechi ya marudiano.
Canavaro alifunga bao pekee lililoipa Yanga ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly katika pambano la kwanza la raundi ya kwanza la Ligi ya Mabingwa Afrika lililopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Canavaro alisema anaamini mchezo wa marudiano utakuwa mgumu zaidi kwa vile wapinzani wao watakuwa nyumbani, hivyo ni wajibu wa kila mchezaji wa timu hiyo kujituma.
“Wachezaji wa Yanga hatutakiwi kubweteka na matokeo tuliyopata katika mechi ya kwanza, Al Ahly ni timu kubwa na mechi ijayo itakuwa nyumbani, hivyo kila mmoja wetu anapaswa kujituma,”alisema Canavaro
Alisema,”Naamini tukijituma na kutumia nafasi tutakazozipata tutawafunga huko huko kwao na hakuna linaloshindikana.”

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>