Nairobi,Kenya
BAADA ya matumaini ya timu ya Zanzibar Heroes kusonga mbele katika mshindano ya Kombe la Challenge yanayoendelea nchini Kenya kufifia, timu ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars imefanikiwa kuitandika timu ya Somalia kwa bao 1-0, iliyofungwa na beki Hemid Mau Mkami,baada ya kupokea krosi ya Erasto Nyoni aliyenasa pasi maridadi ya Ramadhan Singano 'Messi'.
Kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars sasa imefikisha pointi nne na magoli mawili, huku Zanzibar Heroes ambayo jana ilichapwa mabao matatu na Ethiopia na kusalia na pointi zake tatu, ikikabiriwa na ushindani mkali kati ya wenyeji wa mashindano hayo Kenya Harambee stars ambayo inaongoza kundi hilo baada ya kuitandika Sudan Kusini.
Hata hivyo Kilimanjaro Star imejiwekea mazingira magumu ya kupanga matokeo dhidi ya Burundi inayiingia Uwanjani hivi sasa kupambana na Zambia,Burundi katika mechi ya awali iliichapa Somalia mabao mawili huku Kilamanjaro ikotoka sare na Zambia, washambuliaji kama Mrisho Ngassa na Amri Kiemba walikosa mabao ya wazi kabla ya kutolewa nje ya uwanja ,Mabadiliko yaliyoafanywa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen kwa kuwaingiza vijana Haruna Chanongo na Messi iliongeza uhai wa timu na kupata bao pekee la ushindi.