- Ni katika uchaguzi wa ubunge unaowaniwa na vyama hivyo vikuu vyenye upinzani nchini.
Kalenga. Ikiwa siku zinasogea kwa kasi kwa ajili ya uchaguzi wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge jimboni hapa, Dk William Mgimwa, wagombea wa vyama vikuu pinzani wameendelea na kampeni zao kwa kutumia mbinu zenye mvuto wa aina yake.
Mgombea wa ubunge kupitia Chadema, Grace Tendega alitumia mtindo wa kampeni za nyumba kwa nyumba kabla ya kufanya mkutano wa hadhara juzi jimboni hapa.
Huku Chama Cha Mapinduzi (CCM), chenyewe kikiitumia Jumuiya ya Wazazi kumnadi mgombea wa ubunge wao katika Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM, Godfrey Mgimwa kupitia wazazi wa jimbo hilo.
Kampeni hizo zilianza saa 4.00 asubuhi na zilimfikisha mgombea wa Chadema katika Hospitali Teule ya Ipamba iliyoko Kata ya Kalenga jimboni hapa.
Katika kampeni hizo za nyumba kwa nyumba, kulikuwa na makundi mawili ambapo moja liliongozwa na mgombea mwenyewe na la pili likiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Taifa, John Heche.
Katika hospitali hiyo, alitembelea wagonjwa na kuwapa pole. Pia mgombea huyo aliwaomba wamchague ili atatue kero zilizopo.
CCM katika kampeni zao walitumia wazazi wa jimbo hilo ili kusaidia kuleta mabadiliko kwa vijana wao wanaoshabikia Chadema. Katibu wa Wazazi Iringa, Hezron Nganyagwa alisema, wazazi wanaheshimika katika siasa na jamii hivyo kabla mgombea wao hajafika kuhutubia na kujinadi wameona wahamasishe vijana kwanza kupitia wazazi wao.