Raisa Said, Tanga
Rai hiyo imetolewa na Ofisa wa Mfuko huo anayeshughulikia Mradi wa Mafuta kwa Maendeleo (OFD), Novati Kessy katika mkutano maalumu wa asasi za Kanda ya Kaskazini ulioitishwa na WWF kwa ajili ya kujadili uwezekano wa kuanzisha muungano wa kanda kuratibu shughuli za mradi huo.
Kessy alisema kuwa uundaji wa muungano huo wa asasi utasaidia kurahusisha uratibu wa shughuli za utetezi ambazo zimepangwa kufanywa na Mfuko huo ili kuwaandaa wana jamii kwa taarifa sahihi juu ya faida za uwekezaji katika utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta.
Hatutaki kilichotokea Mtwara kitokee hapa kwa sababu kilichotokea kule kilitokana na ukosefu wa taarifa sahihi juu ya uwekezaji katika mafuta na gesi,” alsema Kessy.
WWF imeanzisha mpango uitwao Muunganisho wa masuala ya Mazingira katika utekelezaji wa mpango wa Mafuta kwa Maendeleo ambao una lengo la kujenga uwezo wa asasi za kijamii kufanya utetezi juu ya masuala ya gesi na mafuta.
Chini ya mpango huo, WWF imebuni mbinu ya kufanya kazi na muungano wa asasi katika nagazi za kanda kurahuisha uratibu wa ujenzi wa uwezo katika shughuli za utetezi.
Kessy alieleza kuwa Mpango wa Mafuta kwa Maendeleo ulianzishwa nchini Norway, nchi ambayo imepata mafanikio makubwa katika masuala ya utafiti na maendeleo ya utafiti na mafuta.
mwisho