Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

NA HII NDIO HABARI YA MUJINI BONGO BAADA YA MVUA ZA LEO LIVE!!

$
0
0

 Huwezi kuamini lakini ndo ukweli hii ni mojawapo ya barabara ya mtaa wa Uhuru uliopo maeneo ya Mwenge ikiwa imejaa maji baada ya mvua kunyesha leo mchana lakini kikubwa cha kujua ni kwamba maji haya ni maji ya mvua na hata maji taka maana chemba nyingi eneo hili zilikuwa zikitoka maji hayo machafu.
 Mmoja wa wasamalia wema aliamua kuwapandisha wanafunzi kwenye Toyo yake ili kuwavusha kwenye eneo la barabara lililokuwa limejaa maji mengi eneo la Maghorofa ya JWTZ yaliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

 Gari likipita kwa shida kwenye barabara ya mtaa wa Uhuru baada ya mitaro ya eneo hilo kuzidiwa na kupelekea maji hayo kuanza kupita kwenye barabara hiyo
 Baadhi ya wananchi wakivuka kwa kupita kwenye maji hayo yaliyojaa barabarani 
 Unaweza kusema ni mto lakini eneo hili ni barabara iliyobadilika kwa muda mfupi baada ya mvua kunyesha eneo la Mwenge jijini  Dar es Salaam
 Magari yakipita kwa shida kwenye barabara baada ya maji kujaa barabarani
Mojawapo ya chemba ya maji machafu iliopokaribu na ofisi za TRA ya Kinondoni ikiwa inatoka maji machafu baada ya mvua kunyesha kwenye eneo hilo na kuingia mtaroni.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>