Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

THE MAJANGAZ & BONGO:- SASA WAVUVI WALALAMIKIA MRADI WA GESI MTWARA KUWA NI HATARI KWA KAZI YAO SOMA HAPA LIVE!!

$
0
0


Wachuuzi na wateja wa samaki mkoani wakisubiri kununua samaki. Picha na Abdallah Bakari 

  • Wakazi wa Mtwara ambao baadhi yao wanategemea uvuvi, wanaamini kuwa upungufu wa samaki, umechangiwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya samaki tofauti na uwezo wa wavuvi kulilisha soko la walaji.

Katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili sasa upatikanaji wa samaki wa kitoweo katika pwani ya Bahari ya Hindi, eneo la Mkoa wa Mtwara, umekuwa mgumu.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa makala haya hivi karibuni, umebaini kuwa mabadiliko ya hali ya hewa na zana duni za uvuvi zinachangia hali hiyo.
Lakini wakazi wa Mtwara ambao baadhi yao wanategemea uvuvi, wanaamini kuwa upungufu wa samaki, umechangiwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya samaki tofauti na uwezo wa wavuvi kulilisha soko la walaji.
Pamoja na wavuvi kukiri kuongezeka kwa soko la samaki, wanasema upatikanaji wake umekuwa mgumu hata kwa wale  wanaotumia zana nzuri katika uvuvi.
Wavuvi wanaamini kuwa uchimbaji wa nishati ya gesi asilia imesababisha mabadiliko ya hali ya hewa baharini kutokana na matumizi ya kemikali za kulipua ndani ya bahari wakati wa utafiti na uchimbaji.
“Hapo awali kabla ya kuanza uchimbaji wa gesi asilia baharini, tulikuwa na upepo wa matalai, upepo wa mlaji na upepo wa umande. Pepo hizo zilikuwa mwongozo kwetu kwenye  shughuli zetu za uvuvi,” anasema Ali Hamis Kimbaumbau,  mvuvi na mkazi wa mjini Mtwara.
Anafafanua kuwa pepo za matalai na umande ambazo ni upepo wa kusini huwa ni shwari na zikiambatana na upepo ambao ulikuwa unatoa fursa kwa wavuvi wanaotumia mitumbwi kwenda baharini. Kipindi hicho wavuvi walikuwa wanapata samaki ingawa si kwa kiwango kikubwa.
Anabainisha kuwa kwa sasa pepo wanazopata ni za kaskazi ambazo huambatana na upepo mkali, hali inayozuia wavuvi wenye mitumbwi isiyotumia mashine kushindwa kwenda baharini. Wavuvi wanaofanikiwa kwenda baharini hurudi na mapato duni.
Mvuvi mwingine, Salumu Liwanje (36) anasema wamefikia hatua ya kuamini utafiti na uchimbaji wa gesi asilia baharini ndiyo chanzo.
Anaeleza kuwa siku moja wakiwa baharini, eneo la Luvula walibaini nyaya zenye umeme baharini na walirushwa wakati walipojaribu kugusa maji hayo. Alisema baadaye walisikia sauti ya milipuko mara kadhaa hali waliyodai inaharibu mazingira ya asili ya bahari.
“Joto limeongezeka sana baharini. Hiyo  hali si ya kawaida, ukiingia bahari kuu utakutana na joto ambalo si la kawaida kabisa. Sisi tulizoea nyakati za usiku baharini kunakuwa na baridi kali, lakini hali ni kinyume kwa sasa,” anabainisha Liwanje.
“Unajua wengine tukisema mabadiliko tunayoyaona wapo, watakaosema ni walewale wasiopenda mradi wa gesi. Sasa sisi kama wavuvi tukigusa yale maji yaliyotandazwa nyaya tunarushwa na umeme, je samaki wataishi eneo hilo? ” anahoji mvuvi huyo.
Mkazi wa Kitongoji cha Luvula, Kijiji cha Msimbati, Athumani Mlei (43) anasema pepo za mlaji ambazo zilikuwa zikiwapa mavuno mengi katika misimu miwili sasa hawazipati tena.
“Ile bahari inatetemeka kwa milipuko. Milipuko hii lazima itakuwa ina athari kwa mazingira ya bahari. Kemikali zinazotumika kulipua, lazima zitakuwa na athari kwa viumbe wa baharini na ndiyo sababu pepo mlaji hazipatikani siku hizi,” anasema Mlei.
Mkazi mwingine wa Msimbati Salum, Mussa (62) ambaye ni mvuvi  anasema tangu kutandikwa kwa bomba la gesi kutoka Mnazi Bay hadi mjini Mtwara inayotumika kuzalisha umeme, kina cha maji ya bahari kimeongezeka.
“Tangu litandikwe lile bomba kutoka Mnazi Bay kina cha maji kimeongezeka baharini, hatuwezi kuvua tena kwa mitumbwi, samaki hawapo,” anasema Mzee Mussa.
“Zipo nyumba zilizokuwa kandokando ya bahari ambako zamani maji yalikuwa hayafiki, lakini kwa sasa yanaingia hadi ndani.”
Diwani wa Kata ya Madimba, ambaye pia ni mkazi wa Kijiji cha Msimbati, ambacho kipo ndani ya kata hiyo, Alawi Ali Sadala anathibitisha mabadiliko kwa mifumo ya hali ya hewa, lakini Alawi anasema hatambui kilichosababisha.
“Kweli kuna mabadiliko. Pepo za Mlaji hakuna miaka hii, lakini siwezi kusema ni kutokana na gesi kwa sababu sina utaalam huo,” anabainisha Sadala.
Mmoja wa maofisa anayeshughulikia mazingira wa Kampuni ya Maurel Prom Ltd, ambayo inaendesha shuhuli za uvunaji wa gesi asilia mkoani Mtwara aliyeoomba jina lake lisiandikwe gazetini kwa sababu si msemaji wa kampuni anapinga jambo hilo. Anasema haoni kama kuna uhusiano baina ya uchimbaji gesi na mabadiliko ya hali ya hewa.
“Je na yale maeneo mengine ambayo gesi asilia haichimbwi na mvua hakuna watasema nini, la msingi tukubali kuwa kuna mabadiliko ya hali ya hewa dunaini,” anasema.
Kauli ya wataalamu
Ofisa Uvuvi wa Mkoa wa Mtwara, Gilness Silayo anakiri kuwapo kwa ukame wa samaki kutoka baharini, hata hivyo anakanusha kuwa ukame huo umesababishwa na uchimbaji wa gesi.
“Haya ni matunda ya uvuvi haramu, matumizi ya baruti ambazo huharibu matumbawe sasa madhara yake yameanza kujitokeza, pia mabadiliko ya hali ya hewa, kunapokuwa na jua kali maji ya bahari nayo hupata joto hivyo samaki hukosa utulivu wa kuzaliana.”
“Pia zana duni wanazotumia wakati bahari yetu ina kina kirefu. Hawana uwezo wa kwenda kina kirefu zaidi cha bahari. Sababu nyingine ni ongezeko la wavuvi na uchache wa eneo la kuvua,” anabainisha Silayo.
Anafafanua kuwa hadi sasa mkoa una wavuvi 5,942 ambao hufanya kazi yao katika eneo la kilomita 125 hali ambayo inasababisha wavuvi kupata samaki wachache.
“Idadi hii, ni wale tuliowasajili, lakini wapo wengi ambao hatujawasajili ambao wote wanavua katika eneo moja.”
“Nakubali kuwa hali ya upatikanaji wa samaki ni duni mkoani hapa, lakini si kwa sababu ya gesi. Kama inachangia basi kwa kiwango kidogo sana na hivyo haiwezi kuathiri kwa kiasi hicho,” anabanisha ofisa huyo.
Ofisa wa Mazingira Kanda ya Kusini, Deonis Lyakurwa wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) anasema hoja za wavuvi hao hazina ushahidi wa kutosha na hazina ukweli.
“Haya mambo yanaenda kiimani zaidi. Mbona Dar es Salaam hawachimbi gesi, lakini kuna joto kali? siamini kama miaka hii michache ya uchimaji gesi asilia inaweza kubadili mfumo wa asili wa hali ya hewa ya Mtwara. Hata kama imechangia itakuwa kwa kiasi kidogo sana.
“Kimsingi kuna mabadiliko ya hali ya hewa nchini kote na duniani kwa jumla.  Shughuli za uchimbaji gesi asilia Mtwara na kwingine duniani zinachangia, lakini si suala la Mtwara peke yao. Tatizo ni kwamba mabadiliko haya yamekuja wakati mradi huo nao unatekelezwa kwa mara ya kwanza,” anaeleza Lyakurwa.
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC), Yona Kilagane anakanusha madai hayo kwa kusema: “Si kweli. Hakuna uhusiano kabisa. Kimsingi lazima tukubali kuwa hali ya hewa si tu kwa Tanzania hata dunia kote imebadilika.”

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>