NINI KINAENDELEA DODOMA?
Jana Ijumaa na leo Jumamosi tarehe 07 na 08 Machi 2014
Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma;
Makundi mbalimbali yalitakiwa kukutana jana ili kujenga maridhiano ya vifungu vya 32 hadi 43.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda anaendelea kuongoza jopo la viongozi zaidi ya 20 kutoka kwa makundi mbalimbali na vyama vya siasa katika kujenga muafaka.
Makundi madogomadogo yanaendelea kukutana leo, kisha saa 9 alasiri ya leo tutakuwa na muendelezo wa semina kukubaliana juu ya kanuni hizo.
Tukikamilisha kanuni leo ina maana jumatatu tutazipitisha rasmi, tutafanya uchaguzi na kula kiapo kisha kazi rasmi ya kuijadili rasimu itaendelea baada ya Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba kuiwasilisha.
Utengenezaji wa katiba unahitaji maridhiano ya hali ya juu, unahitaji pande zote zinazohusika zisimamie ukweli, ziache ujanja na mbinu zisizo za msingi, kila kitu kiwe kwa maridhiano na makubaliano ya pamoja.
Nawapongeza wale wote wenye nia njema katika mchakato huu, tusidharau hata kundi dogo lenye manung'uniko, tusitumie idadi ya wengi kuwaburuza wachache, tukae chini na kuelewana, tutambue kuwa Katiba ni ya wananchi, katiba si mali ya waliotumwa kuijadili na kuiboresha.
Mungu Ibariki Tanzania.