Kigali and Pretoria in a Deadly Diplomatic Row: Serikali ya Afrika Kusini iliwapa masaa 72 wanadiplomasia watatu wa Rwanda Nchini Afrika Kusini waondoke haraka nchini humo.Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda nae Loise Mushikwabo ametangaza kuwa Serikali ya Kigali Imejibu mapigo(Retaliation) kwa kuwafukuza wanadiplomasia 6 wa Afrika Kusini nchini Rwanda.
Niliwahi kuonya kuhusu hili mwezi January baada ya kuuawa kwa aliyekua mkuu wa idara ya Ujasusi wa Rwanda aliyekimbilia uhamishoni nchini Afrika Kusini
Sasa jumatatu iliyopita tena Aliyekua Mkuu wa Majeshi nchini Rwanda Jenerali Faustini Kayumba Nyamwasa aliponea kuuwa baada ya nyumba yake anayoishi hukl uhamishoni (Exile) nchini Afrika Kusini kuvamiwa na watu wenye silaha wanaoaminika kuwa ni majususi wa serikali ya Rwanda.Kilichomuokoa na kutokuwepo kwake ndani ya nyumba hiyo tu.Hili ni jaribio la tatu la Mauaji dhidi yake.Mwaka 2010 alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya.
Pia Vyombo vya Dola nchini Afrika Kusini vimewakamata Raia 3 wa Rwanda na Raia 3 waliotangazwa kuwa Watanzania waliohusika na mipango ya mauaji
Sasa wizara ya Mambo ya nje itoe tamko kuhusu hili kama kweli hao waliokamatwa ni raia wa Tanzania na tuchukue tahadhari tusije tukaingia katika mgogoro wa kidiplomasia na Afrika Kusini
Ninaona kuna uwezekano mkubwa wa majasusi wa Kigali kutumia paspoti yetu kuficha uraia wa Rwanda kwa nia mbaya ya kijasusi na kidiplomasia.Natarajia Bernard Membe na au msemaji wa Serikali Assah Mwambene atoe taarifa kuhusiana na hili
Ni kinyume cha sheria za Afrika Kusini na kinyume kabisa na Sheria za Kimataifa kutumia hati za kusafiria,nembo au bendera ya nchi nyingine kufanya uhalifu au kukwepa vikwazo vya kimataifa
Siku chache zilizopita gazeti la serikali ya Rwanda limekua likidai kuwa Tanzania imekua ikiwapa waasi wa FDLR hati ya kusafiria ili kukwepa kutambulika.
Sasa leo serikali ya Afrika Kusini inatangaza kuwa kuna watanzania walioshirikiana na assassins wa Rwanda kufanya jaribio la mauaji ya kisiasa(Assassination Attempt).Hapa kuna kitu,very serious ikiwa utafikiria kwa kina sana
Hali iliyopo sasa ya mgogoro huu mkubwa wa kidiplomasia ambao Rwanda Inaituhumu Afrika Kusini kwa kuwapa hifadhi ya kisiasa(Political Asylum) watuhumiwa wa makosa ya ugaidi dhidi ya serikali ya Kigali ni kitendo cha uadui(Hostility act),Afrika Kusini inajenga hoja kuwa inatenda kulingana na matakwa ya sheria za kimataifa ya kutoa hifadhi za kisiasa kwa kuwa makosa yao ni ya kisiasa na hakuna uwezekano wa watu hao kupewa fair trial watakaporudishwa nchini Rwanda.
Kwa sasa Rwanda na Afrika Kusini zinawajibika kuhakikisha amani inapatikana eneo la mashariki mwa Congo-Kinshasa ambako Afrika Kusini ikishirikiana na Tanzania na Malawi wanechangia kuunda jeshi la pamoja la Umoja wa Mataifa chini ya azimio la Baraza la usalama la Umoja wa mataifa Azimio namba 2098 la kuunda MONUSCO dhidi ya waasi wa M23 wanaosadikiwa kufadhiliwa na serikali ya Kigali
Ni lazima sasa serikali yetu iwe makini hasa kwenye suala hili ambalo raia wake wanatajwa kutumika katika uhalifu huu wa kimataifa na pia kuchunguza uwezekano wa matumizi mabaya ya hati yetu ya kusafiria
Kwa sasa Afrika Kusini imechukizwa na matumizi ya vyombo vya kijasusi vya nchi nyingine kuingilia uhuru na mipaka ya Afrika Kusini na kufanya uhalifu Kinyume na sheria za nchi na pia kinyume na sheria za Kimataifa.

Like· · Share· 3 minutes ago· Edited·