Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MSAJILI WA MAHAKAMA KUU ASHANGAZWA NA KESI YA UMEME WA IPTL SOMA HAPA LIVE!!

$
0
0


Katika kesi hiyo Tanesco ilishtakiwa kwa kukiuka mkataba wa kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya IPTL na shiriki hilo la umeme lilishindwa katika kesi hiyo. 

  • Hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji John Utamwa katika Mahakama Kuu ya Dar es Salaam, Januari 17, mwaka 2014 saa 8: 30 usiku, imezusha maswali kutokana na umuhimu wa Tanesco kwa wananchi wengi.

Dar es Salaam. Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Amiri Musumi ameshtushwa na taarifa kuwa hukumu ya kesi ya Tanesco dhidi ya Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), ilimalizika saa 8:30 usiku.
Hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji John Utamwa katika Mahakama Kuu ya Dar es Salaam, Januari 17, mwaka 2014 saa 8: 30 usiku, imezusha maswali kutokana na umuhimu wa Tanesco kwa wananchi wengi.
Katika kesi hiyo Tanesco ilishtakiwa kwa kukiuka mkataba wa kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya IPTL na shiriki hilo la umeme lilishindwa katika kesi hiyo. Hivyo kupoteza haki ya kumiliki mitambo hiyo kwa asilimia 100. Tanesco kwa mujibu wa mkataba, walikuwa wamiliki mitambo hiyo kwa asilimia zote, mwaka mmoja baadaye.
Hata hivyo, wakati hukumu hiyo ikitolewa jijini Dar es Salaam, kesi nyingine ambayo Tanesco ilishtakiwa na Standard Charted Bank (Hong Kong) Limited huko Washington, Marekani,  kwa kukiuka mkataba wa kushindwa kuwalipa ushuru wa Dola za Marekani 2.5 milioni kila mwezi, ilikuwa ikiendelea ambapo imetolewa hukumu hivi karibuni.
Wakati hayo yakitokea, tayari fedha zilizokuwa zimewekwa kwenye akaunti ya Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa ajili ya kuilipa benki hiyo zimeshatolewa. Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alithibitisha juzi kuchotwa kwa Dola za Marekani 122 milioni (Sh195.2 bilioni) katika akaunti hiyo, lakini akakataa kutaja nani hasa aliyelipwa.
Akizungumzia hukumu iliyotolewa Dar es Salaam, Musumi alisema kuwa ingawa hafahamu sababu za kesi hiyo kuchukua muda mrefu, anashangaa kusikia kuwa hukumu ya kesi ilitolewa saa 8:30 usiku.
“Nadhani kuna watu wameongeza maneno kama unavyojua kuna waandishi wengine wanachukua taarifa kutoka kwa wenzao. Wewe njoo ofisini Jumatatu nitakuonyesha faili la hukumu hiyo, pengine tutajua sababu ya kuchukua muda mrefu,” alisema Musumi na kuongeza kuwa: “Kwa kweli ndiyo nasikia kwa mara ya kwanza kuwa hukumu ilitolewa saa 8:30 usiku.” Alipotakiwa kutoa ufafanuzi, jaji Utamwa aliyetoa hukumu hiyo, alisema kuwa hawezi kuzungumza chochote kuhusu shauri hilo, badala yake  alimtaka mwandishi awasiliane na Msajili wa Mahakama Kuu, kwani ndiye anayeweza kuitolea ufafanuzi.
“Mbona wenzako wameshaandika kuhusu hiyo kesi, wewe ndiyo unataka kuandika leo? Mimi nimeshatoa hukumu siwezi kuizungumzia tena, wasiliana na Msajili wa Mahakama, “ alisema Utamwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>