Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MCHEZAJI MPYA WA SIMBA YAW BERKO ALIPOWASILI JKN AIRPORT LIVE!!

$
0
0






GOLIKIPA Yaw Berko amewataka mashabiki wa Simba kumwamini na kumpa nafasi ya kufanya kazi yake kwani soka ndio ajira yake.

Berko aliyasema hayo wakati alipotua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jana na kupokelewa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo Damian Manembe.

Akizungumza na Spoti Leo Yaw Berko alisema kuwa mpira wa Tanzania anaufahamu vema hivyo yeye hapati shida kwani anajua soka ndio ajira yake na anaamini mashabiki wanakuja uwanjani kutazama timu yao wakitaka ushindi tu.

“Mimi soka ndio ajira yangu hivyo mashabiki wa Simba wasubiri furaha ya ushindi kwani uwezo wangu ni mkubwa  na ndio maana Simba wamemfuata na wachezaji wa kitanzania nawajua uchezaji wao”, alijigamba Berko

Berko amekuja nchini kuitumikia klabu ya Simba kwa mkataba wa miezi sita baada ya Yanga kuvunja mkataba na yeye mwaka mmoja uliopita.


Berko ambaye ni raia wa Ghana ana miaka 33,  alianza kuwa mchezaji wa kulipwa Liberty Professionals FC na kupelekwa kwa mkopo Pisico Binh Dinh F.C 2005-2006 na baada ya mwaka mmoja alirudi Liberty na kupelekwa tena kwa mkopo Yanga 2009-2010.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>