- Kanuni ya 47 ya rasimu za Bunge hilo, zinakataza mjumbe kutumia jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, kwa dhihaka au kwa lengo la kutaka kulishawishi Bunge.
Dodoma. Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Mchungaji Christopher Mtikila, amewaacha hoi wajumbe wenzake pale alipotaka kanuni zisiwabane kuwasema vibaya waasisi wa Muungano.
Kanuni ya 47 ya rasimu za Bunge hilo, zinakataza mjumbe kutumia jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, kwa dhihaka au kwa lengo la kutaka kulishawishi Bunge.
Kanuni hiyo ilimfanya mjumbe wa Bunge hilo, Ezekiah Oluoch, kupendekeza wajumbe wazuiwe kuwasema vibaya marais hao na waasisi wa Muungano waingizwe katika kanuni hiyo.
Hoja hiyo ilionyesha kumgusa Mchungaji Mtikila ambaye alipinga hatua ya kuwazuia wajumbe kuwasema vibaya waasisi hao na kwamba binafsi anaona kama wajumbe wameanza kuwekewa Luku.
“Naona kama tumeanza kuwekewa Luku kwa suala nyeti kama la Muungano, kusema waasisi wasisemwe vibaya au isivyopendeza mimi naona siyo sawa,”alisema Mchungaji Mtikila na kuongeza;
“Naomba hilo liondolewe kabisa ili watu wawe huru kuzungumza juu ya watu wanaowawakilisha kwa mamilioni hapa ndani kwa kufanya hivyo, tutaumia vizuri uhuru wa kujieleza”.
Akijibu hoja hiyo, mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kanuni, Evod Mmanda alisema, kuingiza majina ya waasisi ni jambo lisilowezekana kwa sababu idadi na majina yao hayajulikani.