Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

SUPER STAR MAIMARTHA BAADA YA KUKAMATWA NA POLISI KWA UTAPELI LIVE!!

$
0
0
 Myamarth  akipigwabutwaa mara baada ya kupigwa picha na Camera za Xdeejayz


 Myamarth  hapa akizuga kwa kumuwekea pozi paparazi wetu ili kuharibu muonekano wa kuonekana kukamatwa.

 Hapa kimenuka maofisa wa Polisi wakimuonesha vitambulisho na kumuweka chini ya ulinzi na hakutakiwa kufurukuta.

 Hapa akiwa amechanganyiwa huku Polisi huku kamera za Xdeejayz.

 Myamarth  kwa kuzuga hapa akiweka pozi kabisa na tabasamu.



 Hapa hali ikiwa mbaya akimpigia mumewe simu ili aje kumuokoa.




 "Ndiyo baby nimekamatwa hapa Mwanamboka ndo napelekwa polisi fanya haraka mimi sitaki kuwekwa lupango please sweet njoo haraka"

 Mwanamke aliyeoneshewa mshare ndiye mke wa Kaptein huyo wa Jeshi na pembeni yake ni dada ambae ilidaiwa ni afisa usalama toka Zanzibari ambae alikuja kushiriki kukamatwa kwa Mymartha.




  Gari hii ikiwa imezibwa namba kwa sababu za kiusalama, lakini blog hii inafanya jitihada za kuwatafuta waofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi ili kuzungumzia kama mtangazaji huyo ana uhalali gani wa kutembelea gari hiyo. 
Aliyekuwa mtangazaji wa televisheni tofauti kabala ya kuacha kutangaza na kujikitaa kwenye fani ya umc na biashara Mymatha Jesse wiki iliyopita alitiwa mbaroni kwa kosa la kutapeli shilingi laki tano alizokuwa amepewa kwa ajili ya kufanya kazi ya kusherehesha ndoa ya Kaptein wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania visiwani Zanzibar.
Tukio hilo la kukamatwa mtangazaji huyo zilipendwa lilikuwa kama muvi ya kimafia huku mapaparazi wa Maskani Bongo ambao wakiwa na kamera zao za kisasa zenye uwezo wa kuchukua matukio kwa umbali wa mita elfu moja na kufanikiwa kuchukua picha za tukio zima.
Akiongea na blog hili pendwa namba moja nchini mwanamke anaedaiwa kutapeliwa na mtangazaji huyo aliyejitambulisha kwa jina la Vailet John " 23" alisema kuwa" Nilimpatia pesa za kuja kusherehesha ndo yangu tarehe 11/11/2014 huku ndoa yenyewe ikiwa tarehe 7/12/2013 na nilimpa pesa yote shilingi laki tano hivyo laki tano ilikuwa nje ya nauli na Hotel ambapo nauli ya boti nilimtumia laki moja huku nikimuandalia chumba kwenye Hotel ya kisasa" Alisema mwanamke huyo
Hata hivyo vikao vya harusi vikiwa bado vinaendelea huku kamati ikiwa na matumaini makubwa kwa shughuri yao kufana kutokana na kuongozwa na Mc maarufu na supastaa Mymatha na siku ziliendelea kuyoyoma huku kuikaribia siku ya harusi huku mtangzaji huyo akitoa uhakika wa kuwepo kwenye harusi hiyo.

Zikiwa bado siku mbili ili harusi ifungwe wanakamati hao waliendelea kumsisitiza mtangazaji huyo kuwa anatakiwa kufika mapema ili aonekane kwani wameshamuandalia mapokezi makubwa ikiwa ni pamoja na kumchukula chumba kwenye hoteli ya nyota tatu ijulikanayo kwa jina la Laah Noor ambayo ipo Unguja.
Mwanamke huyo aliendelea kusema siku harusi walimpigia simu Mymatha na kumuuliza kama amenza sagari ya kwenda huko na angeondoka na boti ya saa ngapi" Baada ya kutaka kujua hayo mtangazaji huyo alisema anakuja na ndege mumewe amemwamuru apande ndege, mimi na mume wangu tukaelekea Air Port kwa ajili ya kumsubiri lakini muda ulizidi kwenda huku nikitakiwa kwenda saloon kusuka" Alisema mwanamke huyo kwa uchungu
Baada ya kuona tunamsumbua kumpigia simu sana Mtangazaji huyo alizima simu kabisa hali iliyowafanya wachanganyikiwe kwamu muda ulikuwa umekwenda sana na isingekuwa rahisi kupata Mc Mwingine na mbaya zaidi anasema siku kwenye ndoa waheshimiwa mbalimbali walikuwa wamealikwa wakimwe makanda wa Jeshi la Wananchi wa ngazi za juu pamoja viongozi wa Serikali na Jeshi la Polisi.
Hali hiyo iliwafanya wanakamati kutafuta ufumbuzi kwani tayari ilikuwa saa moja usiku huku saa mbili watu wanaingia ukumbini na wanatakiwa kukaribishwa na Mc, ambapo walilazimika kumtafuta mtu mwenye uzoefu wa kuongea na kumuomba awaondolee aibu kwa waheshimiwa na wakamlipa shilingi laki tatu.

Hata hivyo kwa rehema za Mungu Harusi hiyo ikaisha salama lakini wanakamati ambao wengi ni maofisa wa Jeshi waliokuwa wamejitokeza kumpa sapoti mkuu wao walimsihi mwanamke huyo kumuamuru Mymatha kurejesha pesa hiyo haraka kabla hawajamuwashia moto au kumfuata huku Dar.

Mwanamke huyo anasema amemsihi sana Mymatha kuresha pesa hiyo kwa wanakamti hao lakini mtangazaji huyo aligoma kutoa ushirikiano badala yake alianza kumjibu nyodo mwanamke huyo na hata alipopigiwa simu na Kaptein huyo wa Jeshi aliyefahamika kwa jina la Baraka B Akyo mtangazaji huyo alimjibu vibaya kamanda huyo ndipo chanzo kuundiwa kamati ya kuja kukamatwa.

JINSI ALIVYOTIWA MBARONI
Ilikuwa siku ya Jumanne tarehe 4 mwanamke huyo alikuja Dar akiwa na mwanamke mmoja ambae inadaiwa ni Askari Mpelelezi ingawa hakutaka kujitambulisha ambae ana uzoefu mkubwa wa kuwakamata waharifu wa aina yoyote na baada ya kufika Jijini wakiwa na Rb iliyokuwa inasomeka MZ/RB/29/14 iliyotolewa tarehe 03.03.2014 Uwizi wa Kuaminiwa na kufika kituo cha Polisi Oysterbay kisha wakaongezewa nguvu na wana usalama ambao walianza kumsaka mtangazaji huyo.Wakiwa kwenye gari maalum maalum ambayo yenye vioo tintedi walimpigia kupitia namba maalum na kumwambia mtangazaji huyo kama wanahitaji vifaa vya mkorogo ambapo aliwaelekeza dukani kwake maeneo ya Mitimirefu na walipofika hapo kumbe yeye hakuwepo lakini walichukua vifaa vya mkorofo vyenye thamani ya shilingi laki na elfu tano kisha wakampigia tena kumueleza kama wanaomba awasaidie kuwachanganyia kwani wao ndiyo kwanza wanataka kuanza kutumia mkorogo.

 MYMATHA ANASA MIKONONI MWA WANAUSALAMA KIULAINI
Baada ya mwanamke huyo kumueleza hivyo kama anahitaji kufanyiwa mchanyiko madawa hayo ambapo matangazaji huyo aliwambia kuwa vidonge vyake ni laki mbili je wako tayari kufanya kununua? Mwanamke huyo akasema haina shida atatoa tu hiyo hela basi mtangazaji huyo akawambia kuwa wakutane njia panda ya Kigogo na baadae tena akawambia wakutane kwenye Sheri ya Mwanamboka.

Akiwa maeneo ya Sheri hiyo ndani ya gari moja ambayo inadaiwa ni ya mumewe mwanamke huyo akiwa na vipodozi vyake alishuka kwenye gari hiyo ilikuwa na wanausalama hao na kwa bahati mbaya mtangazaji huyo hamfahamu kabisa mama huyo aliingia ndani ya gari hiyo aliyokuwemo Mymatha kwa ajili ya kuchanganyiwa mkorogo huo.
Akiwa ndani ya gari akijiandaa kuvaa grovu kwa ajili ya kufanya mchanganyo huo ghafra aliona gari yake ikizungukwa na maofisa hao na kumtolea vitambulisho na kumtaka kuelekea kituo cha polisi Oysterbay na wala hakuna swali.
Baada ya kudakwa mtangazaji huyo alimpigia simu mumewe ambae baadae alifika kujitambulisha kama ni Askari kwenye kituo cha Polisi Central na hakuwa anajua chochote kuhusu tuhuma zinazomkabiri mkewe na muda ambao alikuwa amepigiwa simu alikuwa Kibaha akielea Moshi kwenye majukumu ya Kikazi.Hata hivyo paparazi wetu akiwa ndani ya kituo cha Polisi Oysterbay alishuhudia nguvu kubwa aliyokuwa nayo mwanamke huyo na alionekana kuwa na mtandao mkubwa sana wa vigogo wa Serikali kwani licha ya mumewe huyo kufahamika sana kwa maofisa wa polisi  ngazi za juu wa kituo hicho lakini hakufua dafu kwa mwanamke huyo wa Kaptein wa Jeshi kwani tayari kulikiwa na mpango wa mtangazaji huyo kupelekwa Zanzibar kwa ajili ya kujibu tuhuma zake za utapeli na mbaya zaidi kamati ya harusi hiyo ilikuwa haijafungwa wakisubiri hadi apatikane.
 
Mumewe huyo alionekana kuchanganyikiwa ili kumnusuru mama mtoto wake ndipo alipohitaji kujua gharama zote anazodaiwa mkewe ili alipe na lakini sio kupelekwa huko isitoshe mtoto wao hakuwa hali nzuri kiafya. 
Hata hivyo mwanaume huyo alipoambiwa ni gharama zote ni shilingi milioni moja na lakini mbili na sitini usiku huo wa tarehe nne aliingia mtaani kusaka hiyo pesa huku mtangazaji huyo akiwa ndani ya nondo na ilipofika saa sita za usiku mumewe huyo alikuja shilingi milioni moja na kufanikia kumtoa nje mumewe na kuahidi hiyo nyingine atamalizia kesho yake.
Xdeejayz lilimtafuta Mymartha kwaa nia ya simu alipatikana na kukubali kuwepo kwa tukio hilo " Ni kweli huyo mama amenikamata lakini ukweli kwamba nilikuwa sina mpango wa kumdhuruma yeye mwenyewe cheche zake hakuweza kukidhi mashart yangu hivyo nisingeweza kwenda kufanyakazi yake" Alisema mtangazaji huyo ambae amekili kweli laki tano

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>