Kwa mujibu wa mtandao wa Goal.com, nahodha wa timu ya taifa ya Ureno na mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo ndio mwanasoka tajiri zaidi duniani.
Katika listi hiyo iliyotangazwa leo, Ronaldo amerithi nafasi ya kwanza iliyokuwa ikishikiliwa na David Beckham kwa muda mrefu kaba ya kustaafu msimu uliopita. Ronaldo ambaye alisaini mkataba mnono zaidi na Real Madrid miezi kadhaa iliyopita amempita mshindani wake Lionel Messi na mwanasoka anayelipwa zaidi kimshahara Wayne Rooney.