MTU akifanya jambo la kupita kawaida lakini zuri watu husema ‘amekufuru’, yaani amefanya kitu kizuri! Imezoeleka hivyo. Sasa kauli hiyo imekuja baada ya Uwazi kufanya uchunguzi wa kina na kuyabaini mahekalu ya maaskofu wa Bongo kwamba nayo ni kufuru!
Katika uchunguzi huo, Uwazi lilitumia muda wa wiki mbili na kubaini kwamba, watumishi hao wa Mungu wapo vizuri na lile neno wanalolihubiri kwamba, kwa Mungu kuna raha, kwa Mungu kuna maisha mazuri na mtu akiyataka ampokee Bwana!
UCHUNGUZI ULIPOANZIA
Uchunguzi ulianzia kwa askofu mkuu au Nabii George David ‘Geordavie’ wa Kanisa la Ngurumo ya Upako (N.Y.U) lenye maskani yake jijini Arusha ambapo yeye anadaiwa kuwa na jumba kubwa analoishi na familia yake ndani ya jiji hilo na eneo hilo kupewa jina la ‘Mji wa Daudi’. Huyu amewafunika wenzake kwa ubora wa mjengo na pia utajiri alionao.
Habari zinasema mjengo wake huo una mandhari ya kiikulu ukilinganisha na mahekalu ya watumishi wenzake ambao wametajwa kumiliki pia.
Kwa mujibu wa chanzo, mjengo wa nabii huyo aliyejizolea umaarufu kwa kuwa na mfumo wa kiutawala kama ule wa wanasiasa, unapatikana katika Kitongoji cha Njiro, Arusha.
“Sijawahi kuona askofu au nabii anamiliki jumba la kifahari kama lile, lile ghorofa la ofisi tu pia ni balaa. Tena basi ameweka ulinzi mkubwa sijawahi kuona. Nilibahatika kupata picha ya sebuleni kwake utadhani ikulu. Pia niliwahi kuiona ofisi yake jamani! Jamani! (chanzo kinashangaa).
OFISI ZAKE ANAZIITA STATE HOUSE
Chanzo kiliendelea kudai kuwa, ofisi za nabii huyo ni maarufu kwa jina la ‘state house’ (ikulu) ambapo pia hapo analindwa kama enzi za akina Mfalme Daudi ndiyo maana hata sehemu anayoishi panaitwa Mji wa Daudi.
MBALI NA HEKALU
Kwa Nabii Geordavie, mbali na kumiliki utajiri ambao umewahi kuandikwa na gazeti hili siku za nyuma, lakini imebainika kwamba ana kituo cha redio kinachojulikana kwa jina Ngurumo ya Upako FM chenye makao yake jijini Arusha.
MAHEKALU YA WENZAKE
Nyumba za maaskofu wengine ambao walizukiwa na Uwazi ni ile ya Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha Ministry, Askofu Zakary Kakobe wa Kanisa la Zakary Kakobe International Ministry (zamani Full Gospel Bible Fellowship ‘F.G.B.F’).
Maaskofu wengine ni Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ wa Kanisa la Maombezi (G.R.C) Ubungo -Kibangu, Mchungaji Kiongozi Getrude Rwakatare wa Kanisa la Assemblies of God Mikocheni ‘B’ na Mchungaji Christopher Mtikila wa Kanisa la Salvation Church, wanatajwa kumiliki mahekalu mazuri nchini.
MCHUNGAJI GWAJIMA
Mchungaji Gwajima hakamatiki kama Geordavie, kwani anatajwa kuwa na mjengo wenye ghorofa nne maeneo ya Salasala jijini Dar. Gwajima maarufu kwa kurudisha misukule, pia anamiliki magari ya kifahari achilia mbali mabasi yanayotumika kubeba waumini wake kwenda kanisani Kawe jijini Dar.
NABII MWINGIRA
Licha ya kuandamwa na skendo, Nabii Mwingira anamiliki jumba la ghorofa moja Mikocheni B, jijini Dar. Ina ulinzi balaa. Eneo kubwa la jumba hilo ni matumizi ya familia yake.
Pia Mwingira anamiliki Benki ya Efatha iliyopo Mwenge jijini Dar. Anatajwa kuwa miongoni mwa watumishi wa Mungu mabilionea sanjari na baadhi ya viwanja na mashamba anayomiliki.
MAMA RWAKATARE
Mama Rwakatare, wengi humwita ‘Mbaya’. Ni miongoni mwa watumishi wa Mungu waliofanikiwa kujenga nyumba mbili za kisasa, moja ipo Mikocheni B ikiwa na ghorofa moja na Mbezi, Dar yenye ghorofa moja.
MCHUNGAJI MTIKILA
Mchungaji wa Kanisa la Salvation Church, Christopher Mtikila yeye anatajwa kumiliki hekalu moja maeneo ya Mikocheni B jijini Dar likiwa na ghorofa mbili.
MZEE WA UPAKO
Mzee wa Upako ni Mchungaji wa Kanisa la GRC, ni kama Mwingira tu, yeye anamiliki mjengo wa ghorofa moja uliopo Ubungo Kibangu jirani kabisa na kanisa lake.
Mchungaji huyo anatajwa kuwa miongoni mwa watumishi wa Mungu walio vizuri kimaisha. Mzee wa Upako aliwahi kula kiapo katika moja ya vyombo vya habari (jina kapuni) kuwa kwenye maisha yake haamini katika umaskini kwani umaskini siyo sifa nzuri.
ASKOFU KAKOBE
Askofu Kakobe (I.M) anatajwa kumiliki nyumba ya kawaida sana pale Mpakani B, Kijitonyama Dar. Nyumba yake haina ghorofa. Aliwahi kuburuzana mahakamani na baadhi ya waumini kwa madai ya hati miliki ya kanisa.
Jumamosi iliyopita waandishi wetu walifika nyumbani kwake na kubahatika kuzungumza na majirani ambao wengi walikuwa na swali moja ni kwa nini Kakobe hateremshi hekalu la kisasa ilihali fedha anayo?
KUWAPATA ISHU
Miongoni mwa watu wagumu kupatikana na kuzungumza na wanahabari ni watumishi hao wa Mungu ambapo wote walipotafutwa kwa njia zote, simu na kufuatwa makanisani mwao hawakupatikana.
Kuna wakati Mchungaji Lusekelo aliwahi kuulizwa ni kwa nini hawapatikani, alisema hata Yesu alikuwa hapatikani kirahisi!!