Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

DR. SEMAKAFU MBUNGE WA BUNGE LA KATIBA DODOMA NAYE AFUNGUKA LIVE!!

$
0
0



Mimi ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watano ambayo ina mvulana mmoja na wasichana wanne. Nilizaliwa mwaka 1961. Kuanzia darasa la tatu nilisoma katika Shule ya bweni iliyopo Tosamaganga.

Dk. Semakafu: Tunakosea kuligeuza Bunge kuwa vita
Dk. Ave Semakafu amejipambanua kama mjumbe anayepigania usawa wa jinsia bungeni.
Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dodoma. Watanzania wanaofuatilia Bunge Maalumu la Katiba hawatamsahau Dk. Ave Maria Semakafu. Hii ni kutokana na harakati zake katika kuhakikisha kuwa Bunge hilo linazingatia usawa wa kijinsia. Fuatilia makala haya kumjua mjumbe huyo machachari wa Bunge la Katiba.
Swali: Ninaomba unieleze historia yako kwa ufupi.
Jibu: Mimi ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watano ambayo ina mvulana mmoja na wasichana wanne. Nilizaliwa mwaka 1961. Kuanzia darasa la tatu nilisoma katika Shule ya bweni iliyopo Tosamaganga.
Baada ya kumaliza elimu yangu ya msingi nilijiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibosho na baadaye Shule ya Wasichana ya Korogwe kwa masomo ya kidato cha tano na sita. Baada ya hapo, nilijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Nilipomaliza mafunzo yale, nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1983, ambako nilisoma Shahada ya Sayansi ya Siasa katika Uhusiano wa Kimataifa.
Lakini baada ya kutunukiwa Shahada yangu ya kwanza mwaka 1986, niliamua kuunganisha na Shahada ya Uzamili ambayo nililipiwa gharama zote na marehemu baba yangu.
Mwaka 2008 nilihitimu masomo yangu na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Taasisi ya Huduma za Maendeleo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Swali: Kwa kawaida huwa huwa mifano ya watu wenye mafanikio ambao mtu hutamani kufikia malengo yako kama wao, hali kwako ikoje?
Jibu: Baada ya kumaliza masomo yangu niliungana na kikundi cha kujisomea cha IDS (institute of Development Studies) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nawashukuru sana dada zangu Profesa Ruth Meena, Dk. Rose Shayo na wengine wengi ambao wamenijenga na kunifanya nifike hapa nilipo.
Hawa walinichukulia kama mwenzao katika shughuli zao ingawa nilikuwa bado msichana mdogo. Kwa kweli walikuwa nami karibu. Kuwa karibu nao kulinipa hamasa kubwa ya kusonga mbele.
Swali: Unajivunia nini ambacho umefanya hadi sasa?
Jibu: Cha kwanza kabisa ni kufanya kazi vizuri ya uratibu katika Umoja wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (Tango).
Tango walinichagua niwe mratibu wa Mkutano wa Wanawake wa Beijing, kazi ambayo niliifanya kwa miaka miwili. Nilisaidia kukusanya mawazo ya wanawake kwa kuhakikisha kuwa wanawake wa Tanzania wanatoa maoni yao.
Vile vile niliratibu shughuli ya kupeleka wanawake nchini Senegal katika Mkutano wa Wanawake wa Afrika.
Mimi ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya (MUCHS) ambako ni Mkuu wa Idara ya Huduma za Maendeleo. Hizi kazi za uanaharakati unatakiwa kuzifanya kama huduma maana chuoni unatakiwa ufundishe, ufanye utafiti na utoe huduma.
Nimeendelea na harakati hizi na mwaka 1990 tulianzisha kitengo cha jinsia ambacho kilifanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na harakati za uwepo wa usawa wa kijinsia katika vyuo vikuu.
Tumewezesha pia kuanzishwa kwa huduma ya ushauri nasaha katika vyuo vikuu ambazo walikuwa wakituambia kuwa hakuna haja ya kuwa navyo kwa kuwa wanafunzi wote ni watu wazima.
Lakini kwa kufanya tafiti na kuwaelezea kuhusiana na tafiti zilizowahi kufanyika, viliwezesha kuanzishwa katika vyuo vikuu vyote
Swali: Wewe ni Mjumbe katika Bunge Maalumu la Katiba, nafasi uliyoipata kupitia Kundi la Elimu ya Juu. Kwa kifupi kitu gani kimekupendeza katika Bunge Maalumu la Katiba?
Jibu: Mpango wa ukaaji katika Bunge hili umenifurahisha sana kwa sababu unajikuta watu waliozunguka huwafahamu. Ingawa wengine wanaibeza, hii imetusaidia kwa kiasi kikubwa kujenga umoja na kuondoa hofu ambayo tulikuja nayo kuhusiana na Muungano.
Lakini kinachonisikitisha sasa katika Bunge hili ni jinsi tunavyokwamishwa na siasa za vyama. Watu wanafikiria huu mchakato mzima kama vita ya vyama.
Wajumbe wote bila kujali vyama walipaswa kutambua kuwa mchakato huu ni wa Watanzania na tulipoingia ndani ya Bunge hili tulipaswa kujadili mustakabali wa Taifa.
Pia kwa kipindi kifupi nimetambua kuwa wenzetu wa Zanzibar wana jazba sana badala ya kuchangia hoja nzito zinazotolewa, unakuta wanaoongea kwa jazba.
Kunapokuwepo mjadala kwa kawaida hutokea hoja zinazokinzana.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>