Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Makete Shaaban Mkakanze.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya mkutano wa wanachama uliofanyika jumamosi machi 8, mwaka huu kwa pamoja kuazimia kuung'oa madarakani uongozi uliokuwepo baada ya kujadiliana kwa kina katika mkutano huo
Miongoni mwa viongozi waliong'olewa ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Makete Bw. Sahaaban Mkakanze na katibu wake pamoja na uongozi mzima uliokuwa ukiongoza chama hicho wilayani.
Mkutano huo ambao pia uliowashirikisha viongozi wa chadema mkoa wa Njombe akiwemo mwenyekiti Bw. Lulandala, ulibaini kuwa kasi ya kukua kwa chama hicho wilayani Makete ni ndogo ukilinganisha na maeneo mengine licha ya jitihada zinazofanywa na ndiyo maana wakaona wabadilishe uongozi
Katika mkutano huo waliazimia kuchagua uongozi wa muda ambao umepewa miezi miwili ya matazamio kuhakikisha wanakiimarisha chama katika kata zote za wilaya ya Makete ikiwemo kuunda uongozi wa kila kata ambao unaweza kufanya kazi kama inavyotakiwa
Viongozi wa wa muda waliochaguliwa kushikilia chama hicho ngazi ya wilaya kwa muda ni Bw. Ibrahim Ngogo ambaye ni mwenyekiti, Bw. Ilomo ambaye ni katibu na Bw. Stephano Kasanga ambaye ni katibu mwenezi