Jack Dustan ‘Jack Maisha Plus’.
MSANII wa Filamu, Jack Dustan ‘Jack Maisha Plus’ hivi karibuni alinaswa akiwa amevalia nusu utupu huku akiwa bwii kwa pombe.
Tukio hilo la aibu lilinaswa na paparazi wetu ndani ya Ukumbi wa Business Park uliopo Makumbusho jijini Dar ambapo Bendi ya Mashujaa ilikuwa ikiporomosha burudani.
Awali, mrembo huyo alionekana akizama ukumbini hapo akiwa ameongozana na msanii mwenzake, Husna Idd ‘Sajent’ huku akiwa amevaa kigauni kilichoacha mapaja yake wazi.
Moja kwa mjoa walikwenda kuketi kwenye meza iliyokuwa pembeni kisha kuanza kuagiza pombe kwa fujo ambapo ndani ya muda mfupi, al ionekana akiwa tillila hivyo kufanya vituko vya hapa na pale.
GPL