Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimpongeza Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hassan baada ya kuibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake Amina Abdallah Amour. Samia ni Waziri wa Muungano katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Samia Suluhu Hassan ameshinda kwa - 390 sawa na asilimia 74.6 na mpinzani wake Amina Abdalla Amour - alipata kura 126 sawa na asilimia 24 huku kura zilizoharibika ni 7 sawa na asilimia 1.3.
Kwa Muji wa taarifa ya Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Amir Kificho, Viongozi hao wataapishwa Machi 14 2014 saa 10:00 jioni baada ya kuapishwa kwa Makatibu wa Bunge hilo saa nne asubuhi na Rais Jakaya Kikwete.
Sehemu ya wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba wakishangilia wakati wa kumpongeza Mgombea wao Mshindi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan.