Basi la kampuni ya Japanese Express linalofanya safari zake kati ya Makete - Njombe likiwa limetumbukia mtoni mpakani mwa kata ya Lupalilo na tandala wilayani Makete mkoani Njombe, zaidi tazama picha zifuatazo hapa chini.
Katika ajali hii, abiria wameumia na kutibiwa katika hospitali ya Ikonda, hakuna abiria aliyefariki na kwa mujibu wa abiria waliokuwemo kwenye basi hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni basi hilo kukutana na gari jingine kwenye daraja hili jembamba hivyo katika harakati za kumpisha mwenzake ili wasigongane uso kwa uso, ndipo basi hili lilipopoteza uelekeo na kutumbukia mtoni. Basi hilo lilikuwa likitokea Njombe kuja Makete mjini.