Makamu Mwenyekiti wa CCM taifa (Bara), Mzee Mangula akishiriki kuimba wimbo na wanaCCM mara baada ya kuwasili katika kikao cha ndani kilichofanyika katika kijiji cha Mgama.
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kidamali wakati wa kuhitimisha kampeni za ubunge jimbo la Kalenga
Naibu Katibu Mkuu CCM(Bara) Ndugu Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi,kijiji cha Kidamali wakati wa kufunga kampeni za ubunge jimbo la Kalenga
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Seif Shaaban Mohamed akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi na kuwasihi kushikamana katika zoezi la kupia kura ili kuhakikisha ushindi unabaki CCM.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na mjumbe wa Kamati kuu ya Chama chama Mapinduzi (CCM) Bw. Jerry Silaa kushoto akishiriki kuimba nyimbo za kuhamasisha katika mkutano huo wa kampeni aliofanyika kwenye kijiji cha Ibumila kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Simiyu,Njalu Silanga na Anthony Mavunde kutoka Dodoma wakijumuika pamoja.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Sixtus Mapunda akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi kijiji cha Kidamali na kuwaambia Umoja wa Vijana ipo kamili na itahakikisha ulinzi wa kutosha kwa kila mpiga kura.
Mbunge wa Ludewa ndugu Deo Filikunjombe akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi wakati wakufunga kampeni za ubunge ulofanika kjiji cha Kidamali.
Mbunge wa jimbo la Mwibala Ndugu Kange Lugola akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi wakati wakufunga kampeni za ubunge zilizohitimishwa leo kwenye kijiji cha Kidamali na kuwataka wananchi hao kumpa nafasi Godfrey Mgimwa kwa kumpigia kura za ndio siku ya tarehe 16 Machi 2014.
Mbunge wa Viti Maalumu Pindi Chana akiwasisitiza wakina mama kupiga kura kwa mgombea wa ubunge wa CCM Godfrey Mgimwa.
Katibu wa UWT CCM Arusha mjini Ndugu Rehema Mohamed akiwahutubia wakazi wa kitongoji cha Ulete kijiji cha Muwimbi
Chifu Abdul Adam Sapi Mkwawa akiwahutubia Wananchi wa kata ya Nzihi, Kubwa aliloongea ni kuwaomba kumpigia Kura Godfrey William Mgimwa Kwa sababu yeye Kama Chifu amekuwa bega kwa bega na Chama Cha Mapinduzi na ameshuhudia Maendeleo Makubwa yakifanywa na CCM hususani Ujenzi wa Hostel za Wasichana Mashuleni,Umeme,Vituo vya Afya na Barabara zinazopitika wakati wowote.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akihutubia katika kijiji cha Udumka.
Katibu wa CCM Mkoa Wa Mtwara Ndugu.Akwilombe akitoa wito kwa Wanakalenga kuacha kusikiliza Propaganda eti Godfrey William Mgimwa anarithi Ubunge.Amewambia Godfrey amepatiakana katika Mchakato halali wa Kura za Maoni tena ukihusisha wagombea 9.
Kada wa CCM Frederick Mwakalebela na Simon Belege kushoto wakiwa katika mkutano kata ya Nduli katika Jimbo la Kalenga.
Baadhi ya makada wa CCM, kutoka kushoto ni Mtela Mwampamba, Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Salum Mtenga na Akwilombe.
Msanii Dokii akiongoza wakazi wa kata ya Nzihi kucheza nyimbo za kampeni maalumu kwa ajili ya Godfrey Mgimwa.
BILA KUWASAHAU WANANCHI WALIOKUWA WANAJITOKEZA KWA WINGI KWENYE MIKUTANO YA MGOMBEA UBUNGE KUPITIA CCM
Last edited by MwanaDiwani; Today at 11:25.