Mamia ya wasafiri wamekwama katika uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Blantyre, Malawi baada ya uwanja huo kusemekana kutokuwa salama.
Ndege ziliamrishwa kubadili mkondo zikiwa angani hukuwasafiri wakitakiwa kwenda mjini Lilongwe umbali wa kilomita miambili kutoka Blantyre, ili kuendelea na safari zao.
Waziri wa usafiri, Ulemu Chilapondwa, amesema kuwa uwanja huo utafungwa kwa kipindi kisichojulikana kutokana na ubovu wa barabara zinazotumiwa na ndege wakati zikiruka
BBC