Hawaamini: Luis Suarez akishangilia bao la tatu alilofunga katika ushindi wa 3-0 uwanjani Old Trafford
Pengo kubwa: Liverpool sasa wapo mbele kwa pointi 14 dhidi ya Man United na pointi 4 nyuma ya vinara Chelsea.
*********
LIVERPOOL kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mitano iliyopita wamepata ushindi katika dimba la Old Trafford baada ya kuwafumua wenyeji Manchester United mabao 3-0.
Nahodha mashuhuri wa Liverpool na timu ya Taifa ya Uingereza, `Mr. Liverpool`, Steven Gerrard alifunga mabao mawaili, huku bao la tatu likitiwa kambani na Luis Saurez.
Gerrard alifunga kwa penati dakika ya 34 baada ya Rafael kuushika mpira kwa mkono, na alifunga penati nyinginie dakika ya 46 kufuatia Phil Jones kumfanyia madhambi Joe Allen eneo la hatari.
Nyota huyo wa England angefunga mabao matatu `Hat-Trick` katika dimba la Old Trafford tangu mwaka 1936 endapo angefanikiwa kutia kambani penati ya tatu waliyopewa dakika ya 79 baada ya Nemanja Vidic kumfanyia madhambi Daniel Sturridge, lakini alikosa penati hiyo.
Vidic alitolewa nje kwa kadi nyekundu, lakini penati ya tatu inaonekana haikuwa halali kwani Sturridge alionekana katika video akimdanganya mwamuzi na kushinda janja yake.
Kikosi cha Man Utd leo: De Gea 6, Rafael 5,Jones 5, Vidic 5, Evra 5.5, Fellaini 5 (Cleverley 76, 6), Carrick 5, Mata 4.5 (Ferdinand 87), Rooney 4.5, Januzaj 5 (Welbeck 76, 6), Van Persie 4.5.
Kikosi cha Liverpool: Mignolet 7, Johnson 7, Skrtel 8, Agger 7.5, Flanagan 7.5, Henderson 7.5, Gerrard 8.5 (Lucas 87), Allen 8, Sterling 6 (Coutinho 72, 6), Sturridge 8, (Aspas 90+1), Suarez