Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

SHUKRANI WANA KALENGA.......

$
0
0


“Nimejifunza maishani kwamba ujasiri maana yake si ukosefu wa woga,bali ni ushindi dhidi ya woga na kwamba shujaa si yule ambaye hana woga bali ni Yule anayeushinda woga.”Nimeona vema nikianza na nukuu toka kwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Afrika kusini na mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo na afrika kwa ujumla,hayati Nelson Mandela maarufu kama madiba, kufuatia matokeo ya uchaguzi mdogo katika jimbo la kalenga na hali halisi ilivyokuwa kabla ya mbivu kujulikana.

Ni uchaguzi ambao chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) kama ilivyo ada kwa siku za hivi karibuni kwa chama hicho kuchanga karata zake za kisiasa kwa msaada mkubwa wa ‘chopa’ kufuatia umaarufu wao kushuka na mara hii tena walithubutu kufanya hivyo katika aridhi ya Kalenga wakiwa na matumaini chanya juu ya ongezeko la mtaji wa wabunge ndani ya chama chao kupitia uchaguzi huo.

Kwakutumia chopa makamanda hawa wasio na kambi maalumu walifanikiwa kupata idadi kiasi cha watu katika kampeni zao,watu ambao asilimia kubwa walikwenda kushangaa chopa na kuwashanga viongozi wa chama hicho ambao dhahiri shahiri wameshapoteza mwelekeo katika medani za kisiasa nchini,ni idadi hiyo ya watu ndio iliyowapa matumaini hewa viongozi hao na uwepo wa uwingi wa kura kwa upande wao katika siku ya mwsho ya upigaji kura.

Chopa ambayo pengine viongozi hao waliamini ingeleta hofu na woga kwa aliyekuwa mgombea ubunge na mbunge mteule wa jimbo la kalenga  ndugu Godfrey Mgimwa na chama cha mapinduzi kwa ujumla,imani ambayo haikuwa kamilifu kwa wana chadema kwa vile tu CCM walikuwa washindi dhidi ya woga na hofu  waliyotamani  wangekuwa nayo.

Chopa ambayo waliamini kuwa wananchi hususani wapiga kura wa jimbo la kalenga ingewapumbaza na kufanya maamuzi yasiyo sahihi kufuatia woga wao juu ya chopa hiyo,lakini nao wanakalenga wamefanya kitu ambacho mzee mandela alikiamini katika maisha yake yaani kujifunza maishani kwamba ujasiri maana yake si ukosefu wa woga,bali ni ushindi dhidi ya woga na kwamba shujaa si yule ambaye hana woga bali ni Yule anayeushinda woga.

Shukrani wana Kalenga,
Shukrani viongozi wote wa CCM,ama kweli umoja ni ushindi.
Tukutane chalinze

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>