Rais wa Ufaransa na Nigeria, Goodluck Jonathan RFI |
Na RFI
Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa nchini Nigeria amefahamisha jana jumanne kwamba viongozi wameanzisha mkakati mpya wa kusitisha vitendo viovu vinavyoendeshwa na kundi la kislamu la Boko Haram kaskazini mashariki mwa taifa hilo.
Jeshi la Nigeria litaendelea kuendesha vita dhidi ya kundi hilo la kigaidi, ambalo linatuhumiwa kuwamalizia maisha maelfu ya raia tangu mwaka wa 2009, lakini serikali iko tayari kuanzisha “mkakati mpya utaowavuta na kuwakomoa wapiganaji wa kundi hilo”, amesema Sambo Dasuki.
Mkakati huo mpya una lengo la kuzishirikisha jamii katika kupambana dhidi ya kundi la Boko Haram.
“Ninadhani tutashinda vita dhidi ya ugaidi, tukizisihi jamii hizo hasa kuhusu maadili ya utamaduni wetu, dini zetu na kadhalika”, amesema Dasuki, katika kmutano na waandishi wa habari.
Wataalam na mabalozi kutoka mataifa ya magharibi wamekua wakisema mara kwa mara kwamba Nigeria haiwezi ikafaulu kuvunja kijeshi kundi la Boko Haramu, ikiwa uchumi wa kaskazini mwa nchi hiyo utakua bado haujaimarishwa.
Nigeria ni taifa la kwanza kwa uzalishaji wa mafuta katika bara la Afrika, lakini zaidi ya nusu ya raia wake wanaendelea kuishi na chini ya dola mbili kwa siku.
Kundi la Boko Haram, ambalo limedai kuunda taifa la kislamu kaskazini mwa Nigeria, limeendesha mashambulizi mengi kaskazini mwa nchi tangu miaka minne iliyopita.
Chanzo: kiswahili.rfi.fr