Staa Ray C almaarufu "Kiuno Bila Mfupa" akielekea kwenye gari lake mara baada ya kupata dozi yake ya dawa ya kuondoa sumu ya madawa ya kulevya
Kikosi Kazi cha Global Publishers, kimefanikisha zoezi la kumnasa laivu Mbongo-Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, akizama na kuchukua dozi ya dawa za kuondoa sumu ya madawa ya kulevya ‘unga’ mwilini, Amani lina tukio kamili.
Kazi hiyo nyingine nzuri kwa OFM ilifanyika juzi (Jumanne), majira ya saa 3:30 asubuhi ndani ya Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar ambapo staa huyo almaarufu Kiuno Bila Mfupa alifika eneo hilo kwa ajili ya kuchukua dozi hiyo ya dawa aina ya Methadone.