Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

KWA KIFUPI HAYA NDIO ALIYOYASEMA RAIS JK SASA HIVI BUNGENI LIVE BY ZAMARADI KAWAWA!!

$
0
0


Muundo aw serikali Tatu Kama ulivyopendekezwa NA Tume ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba hauwezi kutekelezeka na hautotatua kero NA matatizo yaliyopo katika muundo aw sasa wa serikali mbili.
Rais aw Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameliambia bunge leo kuwa Serikali yake Ina uwezo wa kutatua matatizo ya sasa ya Muungano NA hayuko tayari kwa sasa kukubali muundo aw serikali Tatu labda ije baada ya muda wake aw uongozi.

Amewataka wabunge aw bunge Maalum la Katiba kutafakari kwa kina changamoto zitakazoweza kulikumba taifa iwapo wataamua kukubaliana na mfumo uliopendekezwa aw kuwepo kwa serikali Tatu.

Ametaja baadhi ya changamoto hizo kama zilivyoainishwa na Tume ya Katiba kuwa ni pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa kuwa haina RAslimali zake , vyanzo vya Mapato NA hakuna mfumo aw kulazimisha Nchi washirika kuchangia pale ambapo serikali za Tanganyika NA Zanzibar zitashindwa kuchangia.

Amesema hatari ya kukosa vyanzo vya Mapato ni pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo pamoja NA mambo mengine itashughulikia masuala ya majeshi ya ulinzi NA usalama kukosa mahitaji ya kujiendesha na hivyo kuwepo NA hatari ya majeshi hayo kuamua kujitwalia madaraka katika Nchi hizo kijeshi.

Amesema Hali hiyo ikitokea Nchi haitaendeshwa kwa mujibu wa Katiba NA Demokrasia hivyo amewataka wabunge hao kusoma kwa makini yaliyoandikwa kwenye rasimu na kutafakari kwa kina Athari na faida ya masuala yaliyopendekezwa kabla ya kuyapitisha.

Amesema athari nyingine ni pamoja na kujengeka kwa chuki za utaifa kwani iwapo taifa la Tanganyika litaanzishwa kuna hatari ya watanzania wenye asili ya zanzibar au wazanzibar wenye asili ya Tanganyika kupoteza RAslimali zao walizochuma kwa miaka kadhaa kutokana NA Kuishi katika eneo moja la Nchi iliyokuwa NA Muungano aw serikali mbili kulazimika kurudi katika Nchi ya asili Yao kwa kukosa sifa za kuendelea kuishi eneo Hilo .

Amesema iwapo chuki za kitaifa zitaruhusiwa kuingia nchini NA Watu wabaya wanaweza kuingia hivyo amewataka wabunge aw bunge Maalum la Katiba kutulia na kutafakari kwa makini mapendekezo ya Katiba kwani wana kazi Kubwa ya kubadili NA kuboresha pale inapostahili ili kufanya maamuzi sahihi na kuipa nchi Katiba Nzuri itakayokuwa na maslahi ya wananchi.

Amesema kazi ya Tume ya Katiba imemalizika SIku ambayo Jaji Warioba aliwasilisha rasimu ya Katiba hivyo kazi iliyobaki ni ya bunge hili kuandika Katiba mpya itakayopelekwa kwa wananchi kuipitisha.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>