Mchezaji raia wa Argentina na beki wa zamani wa klabu ya Man United Gabriel Heinze ametangaza kuachana rasmi na soka la ushindani kufuatia majeruhi ya mara kwa mara.Beki huyo ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya Newell's Old boys amesema kila kitu katika maisha kina mwisho wake.
Heinze akiongea hayo kupitia mtandao rasmi wa klabu yake alisema kuwa sehemu ya kikosi cha klabu nzuri ya kiargentina itabaki kuwa kumbukumbu muhimu kwa maisha yake,
"Nataka kusema kwamba mwisho wa msimu huu sitoweza kuendelea kuichezea tena klabu hii,siwezi kupambana tena na maumivu yangu na ninafahamu siwezi kushinda hii vita dhidi ya majeruhi,nilipenda kucheza hadi mwisho wa uhai wangu,lakini nafahamu siwezi kuwa mbinafsi."Gabriel Heinze
Heinze alianzia maisha yake ya soka katika klabu ya Newell's Old ya nchini Aegentina kabla hajatimkia Vallodolid,PSG,Man United,Real Madrid,Marseille na Roma.