Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akihutubia katika hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya Tohara kwa wanaume Mkoani Rukwa iliyofanyika kimkoa katika Tarafa ya Challa Wilayani Nkasi. Akihutubia katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya Mkuu huyo wa Wilaya amesema hadi kufikia mwezi wa tisa mwaka huu 2014 Mkoa wa Rukwa unatakiwa uwe umeshafanya tohara za wanaume 22, 000 ikiwa ni agizo la kitaifa ambapo hadi sasa jumla ya wanaume 7,000 wameshafanyiwa tohara.
Kwa mujibu wa mratibu wa zoezi hilo Mkoani Rukwa tangu kampeni hiyo ianze tarehe 17 Machi 2014 hadi jana tarehe 20 Machi 2014 jumla ya wanaume 583 wameshafanyiwa tohara ndani ya siku 4 katika kituo kilichopo tarafa ya Challa. Kampeni hiyo inaenda sambamba na zoezi la upimaji wa VVU ambapo kati ya wananchi 699 waliopimwa ni mmoja tu amekutwa na maambukizo ya virusi hivyo katika tarafa hiyo ya Challa.
Akizungumzia faida za tohara kwa wanaume amesema husaidia kupunguza uwezekano wa akinamama kupata kansa ya kizazi pamoja na kusaidia kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50%.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akiwasalimia wananchi wa tarafa ya Challa waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni hiyo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Daktari John Gurisha akizungumza katika hafla hiyo. Akizungumzia juu ya zoezi hilo la tohara amesema tohara kwa wanaume husaidia kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanaume kwa zaidi ya asilimia 50%.
Zoezi la Tohara likiwa linaendelea katika zahanati ya Challa.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa awasalimu wananchi wa Challa.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha (watatu kulia), Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Albinus Mugonya (wa tano kulia) na watumishi wa Idara ya Afya katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa (kulia) mara baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)