Straika Wayne Rooneywa Manchester United akishangilia goli lake la pili dhidi ya Aston Villa uliopigwa kwenye uwanja wa Uwanja wa Old Trafford, maskani kwa Man United.
Ndege ikipita juu ya paa la uwanja wa Old Trafford kumpinga kocha wa Manchester United, David Moyes.
MABAO mawili yaliyofungwa na straika Wayne Rooney katika ushindi wa Manchester United wa mabao 4-1
dhidi ya Aston Villa, umempa ahueni kocha wa man United David Moyes ambaye amekuwa akiandamwa na mabango ya kufukuzwa.
dhidi ya Aston Villa, umempa ahueni kocha wa man United David Moyes ambaye amekuwa akiandamwa na mabango ya kufukuzwa.
Mchezo huo, uliopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, maskani kwa Man United, wageni ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 13 Ashley Westwood kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja golini.
Kuingia kwa bao hilo, liliwaamusha Man United kwa kulisakama bao la Aston Villa na kufanikiwa kujipatia bao dakika saba baadaye kupitia kwa Rooney kwa kumalizia kichwa mpira uliopigwa na kiungo Shinji Kagawa.
Wakati Villa wakipigana kusawazisha bao hilo, Mata alididimiza matumaini yao kwa kuongeza bao la tatu katika dakika ya 57, likiwa ni bao lake la kwanza tangu ajiunga na timi hiyo akitokea Chelsea msimu huu.
Chicharito, aliyeingia kuchukua nafasi ya Rooney, alishindilia msumari wa mwisho katika jeneza la Villa katika dakika 90 na kumpa ahueni Moyes ambaye amekuwa akiandamwa na mashabiki wakimtaka kuachia ngazi kutokana na mwenendo wa mbaya wa timu hiyo.