.
pozi na mume wake Gardner Habash ‘Kapteini’ .
Kumbe! Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide amefunguka kuwa yeye na mumewe, Gardner Habash ‘Kapteini’ kwa sasa wanaishi kama kaka na dada hivyo kuibua swali kivipi?Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye
mgahawa wa staa huyo wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Jide alisema kuwa yeye na Gardner wamefikia hatua
ya kuishi katika staili
hiyo kutokana na mapenzi yao yaliyopitiliza.
“Gardner ananipenda sana na mimi pia vilevile nampenda sana mume wangu. Mapenzi
yetu yamepitiliza hadi tunajiona kama vile tumezaliwa tumbo moja na ndiyo maana
nawaambia kuwa mimi na yeye tunaishi kama kaka na dada,” alifunguka Jide.
Ads not by this site
Akiendelea kuzungumza kwa kujiamini, Jide alisema kuwa hadi simu ya mkononi
wanatumia moja kwa ajili ya mawasiliano.
“Mimi hapa sina simu, anayo mume wangu lakini wakati mwingine nakuwa nayo
mimi ila muda mwingi anakuwa nayo Gardner,” alimalizia Jide.
Source:- Bongo Voice Blog