Mwanamuziki wa pop asiyehishiwa vituko kila kukicha, Lady gaga ametoa mpya baada ya kuvaa nguo iliyomuacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake kiasi kwamba unaweza ukaona kila kitu alichovaa kwa ndani wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 28 iliyofanyika katika ukumbi wa ‘Roseland Ballroom’ New York Marekani
”Asanteni sana kwa kujumuika na mimi kwenye bethidei yangu, nilipoamka asubuhi nilikuwa na furaha. Nilikuwa nahamu ya kuwepo hapa usiku huu. Nina marafiki wengi hapa..mashabiki wengi na nimekulia kwa miaka sita” alisema Gaga